Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Hoja ya utekaji, mauaji na kupotea kwa watu ikiwemo watoto imeibuka tena bungeni baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest kutaka mkakati wa Serikali kukomesha matukio hayo aliyodai baadhi yanahusishwa na vyombo vya dola.
Leo Alhamisi, Agosti 29, 2024, hoja hiyo imeibuka bungeni wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, baada ya Anatropia kusema matukio ya utekaji, mauaji na kupotea kwa watu yanaashiria uvunjifu wa haki za binadamu.
Amesema matukio hayo yamekuwa na sura tofauti tofauti ikiwemo wivu wa mapenzi na ushirikina.“Lakini na matukio mengine ya kutekwa na kupotea kwa watu yanahusishwa na vyombo vya dola. Nataka kufahamu mkakati wa Serikali kuzuia matendo haya lakini kuondoa taharuki ambayo inajitokeza katika jamii,” amesema.
Spika Tulia huku akimtaka Waziri Mkuu kutoa kulisemea jambo hilo kwa udogo sana, amesema "Juzi kama mtakumbuka hapa alisimama Mheshimiwa Aida Kenani, mambo haya yanayohusiana na uchunguzi ukiyasema kwa ujumla kwa haya maneno, utekaji, uaji, leo asubuhi nimesoma kuna mganga amezika sijui watu kumi na ngapi. Sasa huyu Mganga ni Polisi au Vyombo vya Dola ambaye watu wazikwa kwake?"
Ameongeza "Unajua haya mambo yakiwa yanasemwa kwa hisia yanaleta picha fulani hivi. Kwa hiyo kuna mtu mwingine anaweza akawa anahisi labda kuna mtu anaroho mbaya mahali hivi, hajali. Kila mtu anajali kila binadamu ana haki ya kuishi lakini tusiweke yale mazingira ya kuonesha kuwa kila anayepotea........kuna watoto si kuna mabasi wanapanda akidondoka chini nyumbani si wanamtafuta? Utasema ni Vyombo vya Dola vimemchukua?"
Ameendelea kusema "Lazima wote tufanye kazi kama viongozi ukichukulia mihemko hautoi nafasi kwa Serikali kufanya kazi yake na wakati huo huo hautoi nafasi kwa jamii kushiriki hili jambo kwani wao watawaza kuna mahali wapo kumbe hawapo sehemu mganga amewazika sehemu. Sisi humu ndani ni Viongozi, tunawakilisha wananchi na tungependa wawe salama. Watu wengine wanahama nchi si tunawapokea hapa, je atasema ni Chombo cha Dola kimewachukua?"
Naye Waziri Mkuu amesema "Tunapoilinda nchi ni wajibu wetu Watanzania wote pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama vyenye jukumu la kupokea taarifa mbalimbali zinazoonesha uvunjifu wa amani popote pale. Na wakishapokea ni kuhskiksha wanafanya uchukuzi na kufikisha kwenye vyombo vya sheria."
Ameongeza "Mheshimiwa Spika nashukuru kwa maneno yako ya msingi ya awali ili kuondoa upotoshaji ambao unaweza kuwa unaendelea na kufanya vyombo vya ulinzi na usalama vishindwe kufanya kazi yake na kuwavunja moyo watu ambao wanafanya kazi saa 24 kwa ajili ya usalama"