Amba Samedi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2024
- 207
- 346
Habari wanajamvi,
Ni jumatano nyingine tena, na nina siku nyingi kweli sijaandika humu.
Katika pitapita zangu, niligundua kuwa wenzetu (Kenya, Uganda na Rwanda) wamepiga hatua kwenye adoption ya vyombo vya moto vinavyotumia umeme: gari, bajaji na pikipiki.
Leo tutazungumzia pikipiki.
Mwezi wa 5, kampuni ya Spiro Tanzania walizindua pikipiki za umeme kwa matumizi hapa nchini. Nilikuwa napitia video yao hapa, nikapata point chache ambazo ningependa kushare na hadhira hii:
View: https://www.youtube.com/embed/vt4w6ulzs6Y?si=zs91YEFdLLTEcgdl
Faida za kutumia pikipiki za umeme (E-Bikes) :
Kazi Kwako: Je, ungetaka kufahamu zaidi kuhusu pikipiki za umeme na faida zao? Una maswali? Nirushie hapa kisa ntayajibu. Asante.

- Kuaga Gharama za Mafuta ⛽
Badala ya kulipa elfu kadhaa kwa petroli kila siku, unabadili betri kwenye kituo cha karibu. Chaji moja inakupeleka umbali wa kilomita 100 hadi 120. Na thamani ya chaji moja ni Tshs 4500.
- Ubadilishaji betri ni dakika chache tu 🔋
Kituo cha kubadilishia betri (swapping station) kinakuwa karibu na eneo lako la kazi. Hauna haja ya kusubiri foleni ya petroli, au kuwaza gharama za juu. (Spiro wanatumia Swapping technology, ambayo inapunguza gharama ya chombo)
Dashboard ya pikipiki ya Spiro. Unaona mwendo, na kiasi cha chaji.
- Matengenezo ni rahisi na ya bei nafuu 🔧
Hakuna gia ngumu au injini za ICE zinazohitaji service kila wakati. Utasahau matengenezo ya kabureta, kubadilisha oil, na mambo yote yanayohusiana na engine ya mafuta.
- Kimya barabarani – hakuna moshi wala sauti 🚫🌫️
Hakuna hewa chafu au kelele. Wateja wako wanapanda kwa raha, na mazingira yanabaki safi.
- Usalama umeboreshwa 📡
Pikipiki zote zina teknolojia ya IoT – Spiro inajua pikipiki yako iko wapi muda wote, na usalama unakuwa wa hali ya juu. Hamna hofu ya kuibiwa. Inatumua software katika uendeshaji, ukilingalisha na pikipiki za kawaida (watu wengi huwa hawawazi usalama wanaponunua pikipiki hizi)
- Gharama za kila mwezi zinapungua sana 💵
Nilikuwa naongea na bodaboda mmoja leo, hapa mji kasoro bahari. Akaniambia kuwa kwa siku anatumia lita 3 hadi 5 za mafuta (kama 10,000 hadi 15,000 hivi). Umbali wa kama 70 had 100 km. Na bado hujapigia hesabu za matengenezo, na kubadilisha oil.
Endapo angekuwa na pikipiki ya umeme kama Spiro, angetumia Tshs 3000 tu, na chenji ikabaki.
Hii ina manufaa sana hasa kwa bodaboda. Utasevu sana kwenye gharama za uendeshaji. Mahesabu tu na kukadiria safari zako. Nilikuwa napiga hesabu ruti kama Morogoro hadi Mzumbe/Mlali. Kwa pikipiki ya mafuta, bila 15,000 hadi 20,000 haendi. Ya umeme je? Nipe 3,000 tupige safari.
- Tayari imeshafanya kazi Afrika 🌍
Spiro imeshaendesha pikipiki hizi Benin, Togo, Kenya, Uganda, Rwanda na sasa Tanzania. Mwamko hapa nchini bado ni mdogo kwa sababu watu hawajauelewa. Ila zikishasambaa mtaani, utumiaji utashika kasi.
Kazi Kwako: Je, ungetaka kufahamu zaidi kuhusu pikipiki za umeme na faida zao? Una maswali? Nirushie hapa kisa ntayajibu. Asante.