Mkuu kama unauza pikipiki za umeme wewe taja faida zake na changamoto zake tuachie sisi
Pili, nimeshamiliki pikipiki za petrol tofauti tofauti lakini sijawahi kutumia Lita tatu kwa km 70
Lita tatu kwa boxes au tvs cc 150 hiyo unatembea mpaka km km 140-150
Boxer na tvs cc 125 hiyo unatembea km 165-180
Pikipiki za umeme ni nzuri lakini zina changamoto zake
Zinapopata changamoto za kiufundi mafundi ni wachache
Na si tu Tanzania duniani bado pikipiki za umeme zina changamoto zake
Ona pikipiki Kali kama Verge TS lakini bado ni changamoto.
Hello kaka,
Asante kwa maoni mazuri. Tukubali kuwa faida kubwa ya pikipiki za umeme ni gharama ndogo. Lita tatu kilomita 150 inategemea efficiency ya pikipiki. Hata hivyo, litre ni 3000, na inaenda umbali wa 50km. 100km ni thamani ya 6000. Bado matengenezo madogo madogo kama kubadilisha oil.
Nna pikipiki ya Haojue old model, na most of pikipiki hapa morogoro ni either Haojue kavu, au Haojue Express kwa sasa. Sidhani kama litre 3 inavuka Km 130 kwa hizi pikipiki za zamani hasa.
Pikipiki ya Spiro iliyotajwa hapo juu ni much simpler ukilinganisha na Verge TS.
Hii nyingine 4100 inakupeleka hizo km 100, na warranty ikiwepo utapata wigo mzuri wa kuifahamu na kujua jinsi ya kuhandle. Tunaweza kujifunza kwenye mass adoption ya hizi pikipiki kule Rwanda, Uganda na Kenya, na changamoto zao. Nimeongea na mafundi wengi katika nchi hizo na kusikiliza interviews. Changamoto zisitufunge macho tushindwe kuona fursa.
Na pia, kama ni issue ya ufundi, tunaweza kuwafundisha fundi wetu jinsi ya kuzitengeneza na kuzimudu. Hii ni fursa ya Africa, na changamoto zote tunazoziona ziwe fursa. EV technology is here to stay. Tuichangamkie mapema.