Mkuu,
Dogo anasema hizo fomu amejaza na criteria ni kwamba uwe na Div 1 a 2 ya A'level. Anasema wanachoambiwa Chuoni wale wote walio na Grant ya Wizara ya Afya ni Kwamba, Hiyo Pesa wao hawatakuja kudaiwa wakimaliza masomo, Hivyo watahitajika kutumikia taifa kwa miaka 5.
Pia wameelezwa na chuo, (KAIRUKI) kwamba Pesa inatoka HESLB as Grant na sio Wizara ya Afya. So kiwango cha Pesa kinachokuja ni Kile kile kama wanachopewa wenye Loans. Tofauti ni kwamba Wao wana Grant na wengine wana Loans! Naomba utupe Uzoefu wako tafadhari, Inawezekana pana wizi unaofanywa hapa kwa wadogo zetu!