Sponsorship

Sponsorship

Mrs chaudevu

Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
21
Reaction score
1
Hellow wanajamii,Naitwa Martha Christian nasoma chuo kikuu Tumaini Makumira Arusha.natafuta sponsorship ya kusoma masters,ninaomba mfadhili wa kunisomesha.popote maana nina nia, namba ni 0657440107
 
hapa watakusumbua 2 dada angu . nakushauri ingia kwenye tovuti znazo dili na mambo hzi. best of lucky i ur life
 
mmmmmmmh!utasumbuliwa mpaka ukome,wengine watakuja bila hata nia ya kweli,kaazi kwako,tafuta means nyingine lkn sio kwa njia hii.
 
Ni pm email yako!, kozi unayosoma na unataka sponsorship ya masomo kwa mwka gn?
Hellow wanajamii,Naitwa Martha Christian nasoma chuo kikuu Tumaini Makumira Arusha.natafuta sponsorship ya kusoma masters,ninaomba mfadhili wa kunisomesha.popote maana nina nia, namba ni 0657440107
 
Rejea mazungumzo yetu PM,nimeona niweke haya hapa labda yatamsaidia na mwingine,Kwanza kama ulivyosema upo mwaka wa kwanza sijaona umuhim wa kuweka jina kamili na namba ya simu coz hakuna atakayekupigia sim akwambie atakupa scholarship leo labda matapeli,Pili nikupe moyo kwamba ni rahisi kupata full scholarship kwa ajili ya kusoma masters kama ukianza mapema kama wewe hivi.Wengi huwa wanafika sehem wanajuta kwanini walichelewa kuanza hizo process.Na nikuambie ukweli shughuli nzima ya kuomba ufadhili kiasi kikubwa haliitaji wewe kujua ubalozi au kampuni au shirika linalotoa sponsorship/scholarship kazi kubwa huwa inakuja umejiandaaje,ukijiandaa vizuri itafika kipindi utakuwa hata hujui uende wapi uache wapi.Kujiandaa ninakomaanisha ni kuanzia matokeo(muhimu sana) japo watu huwa wanasema hata ukiwa na matokeo ya kawaida unapata scholarship but ya kawaida kiasi gani na je utakuwa nayo ikifika huo muda? Nimepitia conditions za scholarships nyingi hadi sasa na karibu asilimia 80 wanataka 'excellent students' japokuwa hawamaanishi uwe wa kwanza au pili au uwe na GPA 4.5 out of 5 but utaona ni jinsi gani matokeo yanaplay part pale mtakapo omba wengi na vigezo vingine vyote mmefanana[\color] kwahiyo ni vema ku'aim higher,do all ur best in class na utavuna mazuri hata kama sio kwa ajili ya scholarship,na hii haimaanishi hapo ulipo kama matokeo sio mazuri basi ukate tamaa NO malizia vizuri kadiri ya uwezo wako(to the maxmum) na utaona matunda yake.
Kingine ni kujiandaa kisaikolojia,anayetakiwa kupata scholarship ni mimi au ni wewe au ni Juma wa Matongo Morogoro na sio someone from Mars or Jupiter,sasa huna sababu ya kuwa na wasiwasi wowote kwamba utakosa coz hazitolewi kwa bahati nasibu[\color] ni suala la juhudi zako unless kama una nyota ya punda kama fulani(joking).
Lugha ni muhimu sana(mitihani),ukiapply masters popote wanataka uwasilishe kithibitisho kwamba unajua lugha fulani,nayo ni mitihani kama ya TOEFl kwa english na TCF,DELF kwa kifaransa,so hata kama una matokeo mazuri ukishindwa kupeleka matokeo ya hii mitihani basi ujue hata kwenye competition haupo.Jiandae sasa coz sio migumu ukizingatia tuna msingi wa kiingereza na hata french kama una muda unaweza kufanya mitihani yake(i knw them).
Kingine ni kufuatilia information kila siku ili kujua vyuo vipya vizuri na namna ya kuapply,kila siku course zinaongezeka na nzuri zaidi pia process za application zinabakidilika sometimes so ni vyema kuwa updated muda wote.Kuwa na tabia ya kuperuzi internet na pia kuuliza kama ulivyofanya.Hii itakusaidia kuwa makini na matapeli(wanaongezeka daily).
Vingine nilivyokutana navyo ni vya kawaida tunaweza kuendelea kudiscuss as time goes on,feel free to ask and to share what u have coz kuna ambao hawajui unavyovijua wewe.
As ulivyosema upo mwaka wa kwanza so hayo yote unaweza kufanya tena vizuri,i wish u the best
 
Back
Top Bottom