Sport Extra ya Clouds wamempotosha Saimon

JFK wabongo

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2015
Posts
3,887
Reaction score
3,197
Wanabodi,
Ni kawaida vyombo vya habari kufanya interview na wachezaji wetu wanaofanya soka lao nje ya nchi. Hivi majuzi hao Sports Extra wamemhoji Msuva. Msuva naye ili kunogesha mahojiano akafunguka mpaka siri za bench la ufundi la timu yake. Siri ambazo ziliisaidia timu yake kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa. Bahati mbaya, Clouds nao wakairusha hiyo habari bila kuchuja kipi kiende hewani kipi kiachwe.

Binafsi nilisikia mpaka masikio yakapata ukakasi. Jambo la faraja ni kuwa interview ilikuwa ya kiswahili na coverage ya radio hiyo ni ndogo. Ila kama ingekuwa radio kubwa na zile timu walizozitoa zikiipata hiyo interview basi zitaweza kukata rufaa kupinga ushindi wa timu hiyo.
Nitoe wito kwa wanahabari, tujitahidi kuwalinda watoa habari wetu. Kitendo walichofanya Sport Extra kinaweza kumchafua mchezaji wetu na kuvuruga ndoto zake za kuwa professional player.
Sijataka kufunguka hizo janja janja ili kutozisambaza zaidi.
 
Ungeweka apa ili wote tujue nini aliongea sio wote tunafuatilia clouds Mkuu.
 
Ungeweka apa ili wote tujue nini aliongea sio wote tunafuatilia clouds Mkuu.
Nikifanya hivyo sitakuwa tofauti na hiyo crew ya Sport Extra ya akina Shafii, Kibwana na Mbwiga. Labda wao wakipata huu uzi waje wathibitishe kuwa walichokirusha hewani hakimpunguzii hadhi mchezaji wetu.
 
Basi naww uache kuleta story za umbea kama huwezi kuweka hapa watu wakasikia kilichosemwa kama kina tatizo
 
Basi naww uache kuleta story za umbea kama huwezi kuweka hapa watu wakasikia kilichosemwa kama kina tatizo
Lengo la uzi ni kuwakumbusha waandishi kuwalinda vyanzo vya habari kwani taaluma yao inawafunza kujua madhara ya habari fulani. Lengo siyo kusambaza walichokitangaza. Ila kama wewe ni mtu wa mpira basi hiyo habari utaipata kupitia njia nyingine.
 
Lengo la uzi ni kuwakubusha waandishi kuwalinda vyanzo vya habari kwani taaluma yao inawafunza kujua madhara ya habari fulani. Lengo siyo kusambaza walichokitangaza. Ila kama wewe ni mtu wa mpira basi hivyo habari utazipata kupitia njia nyingine.
Kama ulikuwa unataka kuwaambia clouds peke yao ungeenda kwny page zao katuka mitandao ya jamii ukasemea huko
 
Kama ulikuwa unataka kuwaambia clouds peke yao ungeenda kwny page zao katuka mitandao ya jamii ukasemea huko
Mkuu, mbona hivyo? una maslahi kwenye hiyo habari? Toka mwanzo naeleza kuwa target ni wanahabari wote sasa wewe unashauri nitumie page za hao hao akina Mbwiga. Page ambazo wanauwezo wa kufuta kile wasichotaka kukusikia. Binafsi nafikiri JF ndo mahali sahihi kwani hawana access ya kuifuta bila kuwasiliana na Moderators.
 
Sasa ungeenda kutoa maoni mwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.!!!! Umezingua
 
Tunataka ushahidi cy ujanja ujanja hapa
 
Nikifanya hivyo sitakuwa tofauti na hiyo crew ya Sport Extra ya akina Shafii, Kibwana na Mbwiga. Labda wao wakipata huu uzi waje wathibitishe kuwa walichokirusha hewani hakimpunguzii hadhi mchezaji wetu.
Basi usingeleta uzi kabisa
 
Msuva yupo sahihi katupa siri kwa nini timu za waarabu hatuziwezi....Sijaona ubaya pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…