JFK wabongo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2015
- 3,887
- 3,197
Wanabodi,
Ni kawaida vyombo vya habari kufanya interview na wachezaji wetu wanaofanya soka lao nje ya nchi. Hivi majuzi hao Sports Extra wamemhoji Msuva. Msuva naye ili kunogesha mahojiano akafunguka mpaka siri za bench la ufundi la timu yake. Siri ambazo ziliisaidia timu yake kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa. Bahati mbaya, Clouds nao wakairusha hiyo habari bila kuchuja kipi kiende hewani kipi kiachwe.
Binafsi nilisikia mpaka masikio yakapata ukakasi. Jambo la faraja ni kuwa interview ilikuwa ya kiswahili na coverage ya radio hiyo ni ndogo. Ila kama ingekuwa radio kubwa na zile timu walizozitoa zikiipata hiyo interview basi zitaweza kukata rufaa kupinga ushindi wa timu hiyo.
Nitoe wito kwa wanahabari, tujitahidi kuwalinda watoa habari wetu. Kitendo walichofanya Sport Extra kinaweza kumchafua mchezaji wetu na kuvuruga ndoto zake za kuwa professional player.
Sijataka kufunguka hizo janja janja ili kutozisambaza zaidi.