Sport Extra ya Clouds wamempotosha Saimon

Lengo la uzi ni kuwakumbusha waandishi kuwalinda vyanzo vya habari kwani taaluma yao inawafunza kujua madhara ya habari fulani. Lengo siyo kusambaza walichokitangaza. Ila kama wewe ni mtu wa mpira basi hiyo habari utaipata kupitia njia nyingine.
For sure...nafikiri ndiyo concern ya mleta uzi.
 
Mkuu, mbona hivyo? una maslahi kwenye hiyo habari? Toka mwanzo naeleza kuwa target ni wanahabari wote sasa wewe unashauri nitumie page za hao hao akina Mbwiga. Page ambazo wanauwezo wa kufuta kile wasichotaka kukusikia. Binafsi nafikiri JF ndo mahali sahihi kwani hawana access ya kuifuta bila kuwasiliana na Moderators.
Mkuu umeeleweka...!
 
Wanabodi,
Ni kawaida vyombo vya habari kufanya interview na wachezaji wetu wanaofanya soka lao nje ya nchi. Hivi majuzi hao Sports Extra wamemhoji Msuva. Msuva naye ili kunogesha mahojiano akafunguka mpaka siri za bench la ufundi la timu yake. Siri ambazo ziliisaidia timu yake kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa. Bahati mbaya, Clouds nao wakairusha hiyo habari bila kuchuja kipi kiende hewani kipi kiachwe.

Binafsi nilisikia mpaka masikio yakapata ukakasi. Jambo la faraja ni kuwa interview ilikuwa ya kiswahili na coverage ya radio hiyo ni ndogo. Ila kama ingekuwa radio kubwa na zile timu walizozitoa zikiipata hiyo interview basi zitaweza kukata rufaa kupinga ushindi wa timu hiyo.
Nitoe wito kwa wanahabari, tujitahidi kuwalinda watoa habari wetu. Kitendo walichofanya Sport Extra kinaweza kumchafua mchezaji wetu na kuvuruga ndoto zake za kuwa professional player.
Sijataka kufunguka hizo janja janja ili kutozisambaza zaidi.
Mkuu umeongea kweli, binafsi hayo mahojiano niliyasikiliza lakini sikuwaza huku ulikowaza Ila umetoa angalizo nzuri sana tena kwa nia njema kabisa ya kumlinda/kuwalinda wachezaji wetu.
 
Msuva hajielewi anaropoka sana sijui ushamba ,manager wake afanye kazi kumuelewesha ase na vitu vya kuzungumza kwenye media ...

Jau sana msuva
Aliyemhoji, mhojiwa, mhariri wa kipindi wote 'manzi ga nyanza'!
 
Wanabodi,
Ni kawaida vyombo vya habari kufanya interview na wachezaji wetu wanaofanya soka lao nje ya nchi. Hivi majuzi hao Sports Extra wamemhoji Msuva. Msuva naye ili kunogesha mahojiano akafunguka mpaka siri za bench la ufundi la timu yake. Siri ambazo ziliisaidia timu yake kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa. Bahati mbaya, Clouds nao wakairusha hiyo habari bila kuchuja kipi kiende hewani kipi kiachwe.

Binafsi nilisikia mpaka masikio yakapata ukakasi. Jambo la faraja ni kuwa interview ilikuwa ya kiswahili na coverage ya radio hiyo ni ndogo. Ila kama ingekuwa radio kubwa na zile timu walizozitoa zikiipata hiyo interview basi zitaweza kukata rufaa kupinga ushindi wa timu hiyo.
Nitoe wito kwa wanahabari, tujitahidi kuwalinda watoa habari wetu. Kitendo walichofanya Sport Extra kinaweza kumchafua mchezaji wetu na kuvuruga ndoto zake za kuwa professional player.
Sijataka kufunguka hizo janja janja ili kutozisambaza zaidi.

Mimisikusikiliza hicho kipindi...ila jambo moja nalifahamu kuhusu tunaowaita waandishi wa habari wa Tanzania,nalo ni kwamba: kiwango cha weledi wa waandishi wetu wa Tanzania kuhusu taaluma yao hii nyeti ni cha chini mno...In fact hata kuporomoka kwa soka yetu waandishi hawa wa habari wana mchango mkubwa wa karibu asilimia 40.
 
Basi naww uache kuleta story za umbea kama huwezi kuweka hapa watu wakasikia kilichosemwa kama kina tatizo

Mtu akitukana mtandaoni na wewe au mwingine akirudia kulisema tusi hilo unadhani itakuwaje???
 
Mimisikusikiliza hicho kipindi...ila jambo moja nalifahamu kuhusu tunaowaita waandishi wa habari wa Tanzania,nalo ni kwamba: kiwango cha weledi wa waandishi wetu wa Tanzania kuhusu taaluma yao hii nyeti ni cha chini mno...In fact hata kuporomoka kwa soka yetu waandishi hawa wa habari wana mchango mkubwa wa karibu asilimia 40.
Kweli kabisa mkuu! Tuna shida sana kwenye hii tasnia.Mfano, wanahabari wanatoa promo kwa wachezaji bila kujali weledi utafikiri wanapromote bongo movie. Promo zao wakati mwingine zinaingilia hata maamuzi ya walimu wa timu ya taifa. Kweli mabadiliko katika sekta ya michezo iendane na maboresho ya tasnia ya uandishi wa habari za michezo.
 
Back
Top Bottom