SportPesa 2018 kufanyika Kenya

SportPesa 2018 kufanyika Kenya

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
7,147
Reaction score
14,699
nondi-edit-1.jpg

Michuano ijayo ya Kombe la Sport Pesa Super Cup, mwaka 2018, inatarajiwa kufanyika Kenya ikishirikisha timu nane za Kenya na Tanzania.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Sport Pesa inayodhamini michuano hiyo, Abbas Tarimba alisema jana wamefurahishwa na ushindani ulioonyeshwa na timu katika michuano ya mwaka huu iliyomalizika juzi kwa Gor Mahia ya Kenya kutwaa ubingwa huo.

Alisema pamoja na changamoto zilizojitokeza kwenye michuano hiyo, lengo lao la kuzinoa klabu kujiimarisha na ligi zao limefanikiwa na wanafurahi kuona hakuna malalamiko ya timu.

Hongera sana Gor Mahia, hongera Zedekiah Otieno (the team coach), hongera Kenya… muiwakilishe vema East africa on the coming match (July 13, 2017) against Everton…
 
I hpe wataleta kikosi cha kwanza...hawa waingereza wana tabia mbaya ya kuleta team B kuchuana na timu za kiafrika...
 
I hpe wataleta kikosi cha kwanza...hawa waingereza wana tabia mbaya ya kuleta team B kuchuana na timu za kiafrika...

Mara nyingi huwa ni kutuondoshea aibu ya kuchabangwa mabao ishini mtungi!

Juzi ile siku Kenya wamecheza na Hull, unaona wangetia kikosi A tungenyukwa mabao sio chini ya thelathini.

Kudumisha urafiki kheri walete kikosi C
 
hata hvo simba sc na yanga sc walidharau sana haya mashandano, walichezesha timu B, na wacheji wa majaribio.
 
hata hvo simba sc na yanga sc walidharau sana haya mashandano, walichezesha timu B, na wacheji wa majaribio.
Hata hizi timu za Kenya kuna vigogo kadhaa walikuwa Serra Leon kwa timu ya taifa Harambe stars
 
Mara nyingi huwa ni kutuondoshea aibu ya kuchabangwa mabao ishini mtungi!

Juzi ile siku Kenya wamecheza na Hull, unaona wangetia kikosi A tungenyukwa mabao sio chini ya thelathini.

Kudumisha urafiki kheri walete kikosi C
emoji23.png
emoji23.png
kuchabangwa mabao sio chini ya thelatini
emoji23.png
emoji23.png
dah!
emoji23.png
emoji23.png
ila ni ukweli, niliona wale wa Hull City Tigers walivyomenyana na sportpesa allstars wakanyukwa mabao na kushindwa ilhali wale wachezaji wa Hull walikuwa bado wachanga sana...kama teenagers vile...dah! sijui Everton team A inaweza ikawatendea unyama upi?
 
Walete team B hao everton waone watakavyo nyoroshwa na k'ogalo
 
Back
Top Bottom