Nimekua nikiona mijadala mingi ya Kenya vs Tanzania ya kutambiana kwa kila namna. Nimechangia katika mada kadha wa kadha hadi pale nilipogundua mijadala hiyo haipo kwa ajili ya kujenga, nikaacha. Niliwaachia wakongwe wa jukwaa hilo nikabaki mtazamaji/msomaji. Katika mijadala mingi wakongwe (wanafahamika sitaki kuwataja) hao wamefanya bila kutukana matusi ya nguo kama ulivyofanya wewe mtoa mada.
Nimesikitishwa sana na kitendo cha kutuita "petty idiots". Ni maneno yenye ukakasi. Sio maneno ya kinywa cha mtu muungwana; labda kama unastahili kuitwa mwana wa kahaba au mwana wa mbwa na majina mengine mabaya ya kuwatukanisha wazazi wako. Wacha mara moja tabia hiyo. Haikuongezei chochote zaidi ya watu kukudharau na kuharibu mijadala yenye tambo za kufikirisha saa nyingine.
Waweza kujifunza kwa member wengi tu hapa wanaotamba na kutambiana bila maneno yenye ukakasi.