SportPesa Super Cup: Yanga kapigwa na timu inayoshika nafasi ya tisa ligi nchini Kenya! Yaaga michuano

SportPesa Super Cup: Yanga kapigwa na timu inayoshika nafasi ya tisa ligi nchini Kenya! Yaaga michuano

Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Posts
1,821
Reaction score
6,119
Dah 3-1 mwenzenu sina Mengi ndo hivyo hali mbaya kwa baba wa Taifa
Yanga jamani,Yanga
--------

Klabu ya Yanga kimeondoshwa katika mashindano ya SportPesa Super Cup 2018 kwa kukubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya timu ya Kakamega HomeBoys, mchezo uliopigwa mjini Nakuru

Kakamega wamejipatia mabao yao kupitia kwa Allan Wanga aliyefunga mawili huku moja likiwekwa kimiani na Opondo. Bao pekee la Yanga limewekwa kiminiani na Matheo Anthony kwa njia ya faulo

Matokeo hayo yanaibakiza Kakamega huku Yanga SC ikiyaaga rasmi mashindano na jumla ya timu 3 sasa kutoka Tanzania ambazo ni JKU, Singida United na Simba SC zikibaki

yanga.jpg
 
tuache ushabiki! toka nianze ushabiki wa mpira sijawah ona yanga au simba mbovu kama hii yanga ya sasa, wanakimbia kimbia tu uwanjan...kama wanafukuza kuku[emoji23] [emoji23]
hahaha!!eti kama wanafukuza kuku aisee nimecheka sn.
 
Dah 3-1 mwenzenu sina Mengi ndo hivyo hali mbaya kwa baba wa Taifa
Yanga jamani,Yanga
--------

Klabu ya Yanga kimeondoshwa katika mashindano ya SportPesa Super Cup 2018 kwa kukubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya timu ya Kakamega HomeBoys, mchezo uliopigwa mjini Nakuru

Kakamega wamejipatia mabao yao kupitia kwa Allan Wanga aliyefunga mawili huku moja likiwekwa kimiani na Opondo. Bao pekee la Yanga limewekwa kiminiani na Matheo Anthony kwa njia ya faulo

Matokeo hayo yanaibakiza Kakamega huku Yanga SC ikiyaaga rasmi mashindano na jumla ya timu 3 sasa kutoka Tanzania ambazo ni JKU, Singida United na Simba SC zikibaki

View attachment 793147
Msijisahaulishe, Kwani mwaka jana Ile timu iliyoitoa Simba kwenye mashindano haya hapa taifa ilikuwa daraja la ngapi huko Kenya ? Kama kuna mpenzi wa Simba atajitokeza kujibu swali hili kwa ufasaha basi huyo ni mpenzi wa soka kwelikweli, siyo hawa wanafiki ambao hujitokeza pale timu inapofanya vizuri, ikichemka wanaingia mitini.
 
... Kwani mwaka jana Ile timu iliyoitoa Simba kwenye mashindano haya hapa taifa ilikuwa daraja la ngapi huko Kenya ?...
Tunazungumzia mchezo wa leo, yaani mwaka huu! Unatetea ujinga wakati Yanga inapoteza mchezo wa saba kati ya 14 iliyopita!
 
Kuna haja ya kuondoa makandokando yote siku ya mkutano mkuu wa chama! Tofauti na hapo timu ijiandae kushuka daraja tu!
 
Msijumlishe na goli za USM Alger.. Mkaja kusema Yanga ni Brazil.
7-1
 
Back
Top Bottom