Waliwahi kusema: HIS SINGLE PASS CAN CHANGE THE GAME.
Andrea Pirlo:
Kabla sijafahamu uzuri Andrea Pirlo akiwa na jezi ya AC Milan, kumbe alipita Inter Milan kuanzia 1998, alicheza michezo 22 tu ya Msimu mmoja wa 1998-1999 kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda Reggina mwaka 1999, na Msimu wa 1999 - 2000 alitumikia tena kwa mkopo akiwa na Brescia, kabla ya mwaka 2001 kuuzwa rasmi kutoka Inter Milan kwenda AC Milan ambapo ndipo na Mimi nilianza kumfahamu na kuvutiwa naye na hatimae kuwa mshabiki wake mpaka kesho.
Fundi huyu wa pass zenye mnyooko wa rula, aliitumikia AC Milan kwa miaka 10 yenye mafanikio kwake na kwa timu pia. Kuanzia mwaka 2001 akivua jezi ya Inter Milan na kuvaa jezi ya AC Milan mpaka mwaka 2011. Kupitia miguu yake AC Milan ilivuna ilichokipanda, kupitia image yake yeye mwenyewe alijivunia alichobarikiwa, kupitia miguu yake tulimtaja kama mmoja ya waitaliano bora kabisa wenye uwezo wa kubadili mchezo kwa pasi yake moja tu...... Alibarikiwa Imani na kubebwa na nyota ya kupendwa huyu ni Andrea Pirlo.
2001-2011 babu huyu fundi wa eneo la kiungo, alifanikiwa kuchukua Serie A mara 2(2004 na 2011), kafanikiwa kuchukua Italian Cup(2004), hakuacha pia Italian Super Cup(2003), akafanikiwa zaidi kuchukua Champions League mara 2( 2003 & 2007), na baadae UEFA Super Cup mara 2(2003 & 2007), Club World Cup. Tunahesabu lakini.....
Hapa Pirlo alituvutia Wengi sana, tukawa teyari tushajenga imani na miguu yake katika kila inachokifanya katika kuugusa mpira mbele ya macho yetu. Nyakati hizo ndizo nyakati ambazo Carlo Ancelotti alikuwa amembadilisha kutoka katika possession aliyokuwa akiicheza kama kiungo mshambuliaji nyuma ya mshambuliaji wa kati, na kumpatia majukumu mapya ya kushuka chini na kucheza mbele ya mabeki wa kati (deep lying playmaker)..... Tukaanza kumuona akianzisha mipira chini na kutuliza timu. Mpaka Leo hii babu huyu mwenye umri wa takribani miaka 38 anacheza katika eneo ambalo mwanadamu Carlo Ancelotti alimwona ndilo eneo lake sahihi.
Baada ya kuweka heshima ya kutosha akiwa San Siro na Giuseppe Meeza. Kuanzia mwaka 2011 mpaka mwaka 2015 Heshima yake iliendelea kubebwa na ubora wa miguu yake. Anakwenda kuvaa jezi ya ndoto zake, jezi ya kibibi kizee cha Turin Juventus. Akiwa na Juventus aliendelea kufanya vile vitu vilivyotufanya tumtaje kwenye mabishano na mijadala yetu vijiweni. Kama kawaida hakuwazidi kuniangusha katika kufufua mipira iliyokuwa imekufa, aliendelea kuwa bora sana katika mipira ya kuvusha eneo la katikati ya uwanja na kumfikia mlengwa( hapa tulimwita mgombanishi).... Okay... Akiwa na Juventus alifanikiwa kuchukua Serie A mara 4, akachukua Italian Cup na Italian Super Cup. Kule Milan walimtaja sana ila huku Turin wakamuimba zaidi na zaidi.
Kabla hajatangaza kuvua jezi ya timu ya taifa ya Italy (Azzuri)..... Alitufanya tumtaje na kumuwaza kama ni miongoni mwa viungo bora ambao wanasumbua akili za makocha wanao kutana na taifa la Italy...... Aina ya uchezaji wake Bado tuna tafuta mtu wa kumfananisha naye, nguvu kidogo ila akili mingi... Akiwa na jezi ya Italy alivutia zaidi katika aina ya uchezaji wake. Nakumbuka mambo mengi sana kuhusu Pirlo na jezi ya timu ya taifa ila Pole penenka dhidi ya Joe Hart. ...
Tangu 2002 mpaka 2015 (116 caps, 13 goals: akiwa kachukua World Cup) akiwa na jezi ya timu ya taifa ya Italy. Hiyo imetosha yaliyobaki yakiobaki tutasimuliana kwa mdomo tuache maandishi yapumzike....
New York city fc..... Ndio sehemu aliyopo hivi sasa
Na teyari ameshatangaza kuvua viatu vyenye Meno sita, baada ya kuvua jezi ya Inter Milan, AC Milan na
Juventus.... Na sasa anataka kutundika jezi yenye Etihad kifuani katika enga ya geto na kurudi kuishi kama binadamu wa kawaida... Baada ya kucheza michezo 715 ngazi ya klabu, 116 akiwa na jezi ya Italy na kufunga magoli 86 pamoja na kushinda vikombe 18.
Jiandae Pirlo kudondosha chozi... Miguu yako ni rafiki wa mpira ule wa duara na hautolia mwenyewe mpira nao utatoa chozi kabla ya wewe kupokea Maua kutoka Milan, Turin na New York. Najua utatumis ila nasi tutakutaja sana katika mabishano yetu vijiweni....
Respect .....
HK