Sports arena ya wasafi: Hatutamuita zahera

Hiv karibuni Mwinyi Zahera amekuwa akifanya media tour na kuwalikwa pia na media mbalimbali sports arena wameulizwa mbona wao hawajamwita Zahera wamejibu "Zahera ameshafukuzwa na yanga na kocha anapimwa kwa matokeo au uchezaji wa timu yake hatuna sababu yakumwita studio hata ukimwita azungumzie yanga itakuwa Haina faida sisi hatufanyi kazi za umbeya labda ingekuwa tunafanya mahojiano ikiwa yupo ndani yanga ndio ingekuwa inamake sense".
ogopa sana mke ambaye mkiachana anaanza kukutangaza mtaani...
 
Hao sports Arena wana akili sana. Na bila shaka wameonesha ukomavu! Ni uwendawazimu kutengeneza vipindi na mtu ambaye ameshafukuzwa kazi, kwa lengo tu la kumchafua na kumdhalilisha mwajiri wake.

Hayo malalamiko si angeyatoa kabla hajafukuzwa? Atatumiwa na hizo media, mwisho wa siku ataenda tena kuwapigia magoti hao hao viongozi ili wamlipe stahiki zake.

Na ningekuwa mimi ndiyo Mwenyekiti wa klabu, ningehakikisha anayapata hayo malipo yake kupitia Tff, Caf, Caz, au Fifa kabisa.
Kwa njia zote lazima atalipwa,.. ubaya wake ni upi?
 
Amefukuzwa kazi, akae kimya, asubirie stahiki zake, aondoke zake na kwenda kutafuta changamoto mpya! Makocha wenzake wote nchini na duniani, hufanya hivyo! Yeye siyo kocha wa kwanza duniani kufukuzwa.

Kama anahisi ameonewa, kuna vyombo husika vya kudai haki! Huko kulialia kwenye vyombo vya habari hakuwezi kubadilisha chochote! He is fired!
 
Hiv karibuni Mwinyi Zahera amekuwa akifanya media tour na kuwalikwa pia na media mbalimbali sports arena wameulizwa mbona wao hawajamwita Zahera wamejibu "Zahera ameshafukuzwa na yanga na kocha anapimwa kwa matokeo au uchezaji wa timu yake hatuna sababu yakumwita studio hata ukimwita azungumzie yanga itakuwa Haina faida sisi hatufanyi kazi za umbeya labda ingekuwa tunafanya mahojiano ikiwa yupo ndani yanga ndio ingekuwa inamake sense".
mko very bright, hongereni msijifananishe na mbumbumbu wa Clouds fm na efm
 
Amefukuzwa kazi, akae kimya, asubirie stahiki zake, aondoke zake na kwenda kutafuta changamoto mpya! Makocha wenzake wote nchini na duniani, hufanya hivyo! Yeye siyo kocha wa kwanza duniani kufukuzwa.

Kama anahisi ameonewa, kuna vyombo husika vya kudai haki! Huko kulialia kwenye vyombo vya habari hakuwezi kubadilisha chochote! He is fired!
We kama nani unamzuia kuongea..? Mtu mzima unampangia chakufanya..?
Kwani akiongea anawatoa nini.. Acha aongee then atanyamaza.
Huna mamlaka juu ya kinywa chake.. Tuache ushamba mkuu
 
Hakuna wa kumzuia! Isipokuwa tunamshauri tu aachane na uvuvuzela wake maana hautabadilisha chochote! Ameshafukuzwa kazi! Hivyo ni wakati wake wa kwenda kutafuta changamoto mpya, badala ya kulialia kwenye hizo media.

Anachokifanya Zahera ndiyo ushamba wenyewe! tena uliochanganyika na utoto ndani yake! Yanga ilikuwepo kabla yake, na itaendelea kubaki kwa miaka mingi tu ijayo bila yeye. Utoto anaoufanya, utampotezea hata ile heshima ndogo aliyoipata kwenye timu yetu.
 
Back
Top Bottom