Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Miradi ya mingi ya TARURA ina matatizo ya usimamizi.
Makandarasi walio chaguliwa kwenye tenda za TARURA wengi ni wababaishaji na hivyo kukosa viwango vya kutekekeza miradi.
Waziri Mkuu Majaliwa kalionyesha hilo wazi baada ya ukaguzi wa barabara huko Ukerewe.
Mkandarasi kapewa siku kumi na mhandisi msimamizi, Waziri Mkuu kamwongezea tano kabisaa, kuwa siku kumi na tano.
Hilo safi kabisa maana sasa mpira umewaangukia TARURA, huyo mkandarasi waliyempa tenda kama ni kanjanja, hataweza kukamilisha huo mradi in 15 days.
Majuzi huko Morogoro, kuna mkandarasi aliyekuwa akijenga daraja, alifutika michanga na vipande vya mbao badaka ya zege.
Hizo ni dalili zote za kukosa usimamizi wa kitaalam toka TARURA.