Spotify yatangaza ngoma na wasanii wa Tanzania waliosikilizwa zaidi mwaka 2024. Marioo ashika usukani!

Spotify yatangaza ngoma na wasanii wa Tanzania waliosikilizwa zaidi mwaka 2024. Marioo ashika usukani!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Kama mnavyojua kuwa tuko mwishoni kabisa mwa mwaka 2024 na hivi karibuni mtandao wa kusikilizia muziki ambao una makao makuu yake huko USA, umetoa orodha ya wasanii kutoka Tanzania waliofanya vizuri zaidi.

Kwenye list yao, Spotify wametoa orodha ya wasanii, album na ngoma zilizofanya vizuri zaidi kwenye mtandao huo huku wasanii kama Marioo, Diamond Platnumz, Jaivah na Harmonize wakiwa wametajwa.

======================================================
Kati ya wasanii 10 waliosikilizwa sana nchini Tanzania, wanne kati yao ni wasanii wa Tanzania na 6 (sita) ni kutoka nchini nyingine barani Afrika.

Ndani ya kumi bora, nafasi ya pili, ya tatu, na ya nne kwa wasikilizaji wa Tanzania imeshikwa na Marioo, Diamond Platnumz, na Harmonize. Huku Alikiba akiwa msanii mwingine wa Tanzania katika orodha hiyo akishika nafasi ya 10.

Data hizi zinaonyesha kwamba wasikilizaji wa mtandao wa Spotify nchini Tanzania wanasikiliza sana wasanii wa barani Afrika, wakiwa na wasanii wanne kutoka Tanzania kati ya 10 bora waliosikilizwa sana


Spotify 2.png
“Hakuna Matata” wa msanii Marioo ulikuwa wimbo pendwa mwaka huu kutoka Tanzania

Wasanii waliosikilizwa zaidi Tanzania Spotify mwaka 2024
  1. Chris Brown
  2. Marioo
  3. Diamond Platnumz
  4. Harmonize
  5. Drake
  6. Asake
  7. Ayra Starr
  8. Burna Boy
  9. Davido
  10. Alikiba

Nyimbo zilizosikilizwa zaidi Tanzania Spotify mwaka 2024

  1. Commas - Ayra Starr
  2. Lonely At The Top - Asake
  3. Hakuna Matata - Marioo
  4. Mapoz (feat. Mr Blue & Jay Melody) - Diamond Platnumz
  5. Tshwala Bam (feat. S.N.E & EeQue) - TiToM, Yuppe
  6. Angel Numbers/Ten Toes - Chris Brown
  7. American Love - Qing Madi
  8. Komasava (Comment Ça Va) - Diamond Platnumz, Khalil Harrison, Chley
  9. Egwu - Chike
  10. Buruda - Jaivah, Marioo

Nyimbo za wasanii wa Tanzania zilizosikiizwa zaidi Spotify mwaka 2024

  1. Hakuna Matata - Marioo
  2. Mapoz (feat. Mr Blue & Jay Melody) - Diamond Platnumz
  3. Komasava (Comment Ça Va) - Diamond Platnumz, Khalil Harrison, Chley
  4. Buruda - Jaivah, Marioo
  5. Zawadi - Zuchu, Dadiposlim
  6. Dharau - Ibraah, Harmonize
  7. Baridi - Jay Melody
  8. Siji (feat. Toss) - Zuchu, Toss
  9. Nisiulizwe - Jux
  10. Away - Marioo
 
Back
Top Bottom