Spring of Sadness - Eric Shigongo

Spring of Sadness - Eric Shigongo

Ni kwelindugu uko sawa kabisa maana neno Kisima kwa Kiingereza ni WELL, na neno SPRING linatafsiriwa kama " A place where water wells up from underground source", Kwa maana hiyo ni upotoshaji mkubwa! Achana na huyu kilaza MICSIMON, hajitambui! labda sina hakika kama alitaka hadithi yake ilete maana labda angeandika " A WELL OF SADNESS", au labda alikuwa akitaka kusema "KISIWA CHA HUZUNI"!
 
Spring of sadness~ maana yake ni kijito cha huzuni na c kisima cha huzuni
 
Nyie mnalumbana mwenzenu Shigongo anaingiza PESA!
 
Wakuu,

Naombeni msaada wenu kwenye hili na ikiwezekana toeni ushauri wenu kwa huyu Bwn. Shigongo, kwangu kama nimepituka na Watunzi wengine wa hadithi na sinema za Kitanzania na kuzipa majina ya kiingereza.

Mimi binafsi sio mtaalam wa lugha hiyo ya kiingereza ila kwa kiasi fulani naweza kugundua kosa.

Juzi hapa nilisoma katika gazeti la Risasi kama sikosei huyo Bw Shigongo ameandika hadithi humo na kuipa Jina la SPRING OF SADNESS na kuitafsiri kwa kiswahili kwa KISIMA CHA HUZUNI.

Kwa maana halisi ya hicho kingereza hapo yaani SPRING ni tofauti kabisa na maana mgeuzo ya KISIMA kwa kingeleza.

Kisima ni maji yaliyo tulia tofauti kabisa na spring,spring ni maji yaliyo katika kububujika au kutiririka.

Nadhani Bwn.Shigongo angetafuta watu wanao jua lugha hizo vizuri akawapa kazi ya edit hadithi zake na kuzirekebisha pale inapo bidi,na si tu kuziweka kwenye kurasa.

Magazeti yake yanasomwa na watu wengi, wengine wapo katika kujifunza, sasa unapomwambia spring ni kisima na kubeba hiyo maana, then atabisha hata kwenye ukweli akiaambiwa spring si kisima.

Na kama mimi ndio nisiye elewa hapa basi tafadhali nielimisheni

Hivi kisima kinaweza kuwa na maji yaliyotulia halafu source yake ni nini? yaani hayo maji yaliyotulia yametoka wapi ndo yakaenda kutulia kwenye kisima? Mimi ninavyojua huwa kuna visima vya asili ambavyo mara nyingi vinakuwa vifupi na vinakuwa sehemu ya chemchemi hivi nadhani kwa kiingereza huitwa spring, na kuna visima virefu ambavyo mara nyingi huchimbwa kitaalamu na kabla ya kuchimbwa lazima tathmini ifanyike kama kuna maji ya kutosha na kikishachimbwa kukawa na maji ya kutosha na hapa maji pia hububujika toka chini na urefu wa kisima hutegemea na jinsi water table ilivyokaribu kutoka uso wa dunia, visima hivi huitwa wells kwa kiingereza.
 
Kwa maana hiyo unasema "Spring of Sadness" ya bwana Shigongo ilipaswa itafsiriwe kama "Chemchemi ya huzuni" na sio Kisima cha Huzuni kama ilivyo sasa!
 
Kwa maana hiyo unasema "Spring of Sadness" ya bwana Shigongo ilipaswa itafsiriwe kama "Chemchemi ya huzuni" na sio Kisima cha Huzuni kama ilivyo sasa!
Labda 'kisima cha asili cha huzuni' ha ha ha ha nilikuwa nawaza tu kwa sauti bahati mbaya umenisikia. kizungu kigumu jamani na kina maneno mengi. Offcourse angetumia 'Chemchemi ya huzuni' pengine ingekuwa sahihi au 'bubujiko la huzuni' ingeweza kuwa sahihi pia, lakini hata 'kisima cha huzuni' bado sio tafsiri mbaya.

Maana ukisoma kwenye baadhi ya kamusi za kizungu "spring---to arise or result from", hapa tafsiri yake kwa kiswahili ndo kububujika. Na nyingine pia "spring---a small stream flowing out from the ground", hapa kiswahili chake ndo Chemchemi.

Lakini mimi nashawishika kusema hata kisima sio tafsiri mbaya kwa sababu msingi wa kisima chochote ni maji kutoka ardhini kuja juu.
 
Mkuu Masuke asante sana, ngoja nikubaliane na wewe kuwa labda hata tafsiri ya kisima sio mbaya sana(hii ni baada ya ufafanuzi wako), lakini tabu yangu ni kuwa vijana wetu wengi siku hizi hawana tabia ya kujisomea na kutafuta usahihi wa jambo, na wengi wao ndio hasa wasomaji wa hadithi hizi za Shigongo, sasa inapokuwa hakuna tafsiri sahihi hasa kigramatia (grammartical interpretation) inaleta tabu kwa vijana hawa kujifunza hizi lugha za wageni!
 
Back
Top Bottom