Sriracha inapoteza Mapato ya Billion 4.3 Kila mwaka kwa kutokusajili TRADEMARK

Sriracha inapoteza Mapato ya Billion 4.3 Kila mwaka kwa kutokusajili TRADEMARK

Luhamba II

Senior Member
Joined
Mar 22, 2025
Posts
137
Reaction score
219
Kabla sijaeleza jinsi Sriracha inavyopoteza pesa ngoja nikupe background fupi ili uelewe Sriracha ni nini.

Mwaka 1979 wakati vita ya Vietnam imeshamiri, watu wengi walikua wakikimbia Vietnam kuelekea mataifa ya ulaya na Amerika.

Moja ya watu waliokimbilia upande wa Amerika ni bwana mmoja wa makamo anaitwa David Tran.

David Tran akafikia marekani Jimbo la Los Angeles mwaka huo 1979.

Mwaka unaofuata February 5, 1980 David Tran akaanzisha Kampuni yake ya chakula kwa jina la "Huy Fong Food"

Kwakua yeye ni mpishi mzuri tokea Vietnam biashara ilimuendea vizuri.

Moja ya bidhaa ya Kampuni yake ilikua ni Hot sauce (pilipili chachandu) kwa jina la "Sriracha"

Kwahiyo kwa mara ya kwanza Dunia ikasikia neno Sriracha.

Mauzo ya Sriracha yalikua yanafikia chupa Million 20 kwa mwaka na kuingizia Kampuni mapato ya $2300 kwa mwezi.

Mwaka 2004 Kampuni zingine vya vyakula zikaanza kuingizia supermarket pilipili sauce kwa jina Hilo Hilo la Sriracha.

Na kwakua watu walikua wakiipenda Sriracha walikua wananunua tuu bila kufikiria mara mbili.

Supermarkets zikawa flooded Sriracha kila Kona alafu zote sio za Mzee David Tran.

Kampuni mama ya Tran ikaanza kupoteza pesa kutokana na ushindani wa soko.

Swali la muhimu hapa ni kwanini Sriracha haikusajiliwa kama trademark?

Hakuna mtu anajua.

Huenda Mzee David hakua na elimu ya mambo ya Trademark na Intellectual property laws.

Au alichagua njia ya amani.

Au hakua na mwanasheria.

Kufikia mwaka 2014 Kampuni ya Huy Fong Food ikapoteza umaarufu wake huku Sriracha zikiingia nyingi na isijulikane ipi ni ipi.

Listen, haijalishi brand yako Ina influence kiasi gani, kama haujasajili Trademark utapoteza nguvu yako sokoni.

Hey naitwa Luhamba Mimi ni mwanasheria na agency freelancer nawasaidia wafanya biashara kama wewe kusajili trademarks, patents, biashara na Kampuni.

Kama unahitaji consultation zaidi kuhusu usajili wa trademark unaweza kunitumia ujumbe WhatsApp kupitia namba hizi

0678131068

Your Favorite Lawyer.
 
Back
Top Bottom