SSD 128 itatosha kwa windows

SSD 128 itatosha kwa windows

Nyamwage

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2020
Posts
712
Reaction score
1,748
Nina HDD 1tb nimeongeza na 128gb SSD kwa ajili ya Windows na system ili kuwezesha PC kuwaka haraka na kweli mabadiliko nayaona PC inawaka haraka na inakuwa tayari kwa matumizi bila ya kuirefresh nimeweka na game moja humo kwenye 128 SSD lina 28 gb tangu hapo sijainstall kitu chochote humo kwenye disk.C zaidi ya updates za windows na security mwanzo nilibakiwa na 48.6gb siku iliofuta zikawa 47gb siku nyingine tena 45.6gb leo naona imebaki 45gb wasiwasi wangu ni kwamba hii SSD itajaa soon
 
Inatosha ila ndio huko kujibana Bana. Inapungua space sababu game lina save, programs nyengine kama browser unaweka temp files etc. Baadae unaweza kuja kuvifuta na ku clear nafasi.

Sema siku hizi ssd zimeshuka bei sana, ukipata deal zuri ongeza ukubwa
 
Haitoshi mkuu, angalau ingekuwa 256 GB. Hiyo itajaa muda mfupi sana
 
Clear temp. files kabla hujajipanga kuongeza SSD...
 
Usiweke game kwenye C hapo itatosha vizuri, C weka windows na programs tu.
Lakini pia drive zidhani kama zina gharama tofauti sana ungetafuta ya 256 au hata 1TB ukijipanga.
 
Back
Top Bottom