St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Kwanza ili kuingia shule Kuna mtihani wa mchujo, watoto hua wengi Sana zaid ya buku 3 na wakachukua watoto 100 hivyo ni bright haswaaa hili ndilo kubwa kuliko yote. Mazingira mazuri ya kujifunzia, kuwakeep wanafunzi busy katika kipindi chote Cha masomo mpka muda wa likizo.

Kipindi Cha likizo wanapewa home package, Ni maswali mengi watoto hufanya mpaka tarehe ya kufungua na bado hawajamaliza.

Hili la kununua mitihani ni uzushi na halina ukweli hata kidogo. Mtoto aliyekua wa kwanza kitaifa ni ndugu yangu wa karibu, Consolata toka akiwa shule ya msingi alikua bright Sana. Shule ya msingi aikwa darasa la tano alishinda tuzo ya kuandika insha na lilikua shindano la shule zima, toka hapo tukajua sio mtoto wa kawaida. Hili la kuingia wa kwanza kitaifa sio kwamba limekuja tu, alikua anajua na amejiandaa kuingia 10 Bora kitaifa. Hata mtihani wa mock alikuwa wa kwanza kwa Kanda.

Mwisho naweza kusema watoto wengi wa st Fransis hua ni bright, lakini pia hupata malezi bora shuleni na nyumbani.
 
Hapo kwa Consolata panaweza pakawa kamba ili kulazimisha hoja sema nn mm nimekupata hivyo hivyo
 
Binti anataka kutuaminisha kakulia mummy this daddy that families kumbe mmatumbi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hapana anaweza asiwe na maana hiyo labda , wengi lugha zetu za kwanza ni lugha zetu za makabila alaf kiswahili lugha ya pili mimi nimemuelewa kwa upande huo. Mfn kuna maeneo mimi hukwepa kutumia msamiati wa kiswahili kutokana na kusumbuliwa na matumizi sahihi ya silabi L& R. Lakini kama alimaanisha hakiwezi kiswahili hiyo hapana [emoji23][emoji23]
 
Hivi kweli lugha ya kwanza iwe kihehe afu umudu standards za St Francis mbona hiyo kamba🀣🀣🀣🀣
 
Hivi kweli lugha ya kwanza iwe kihehe afu umudu standards za St Francis mbona hiyo kamba[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yah inawezekana kiswahili na lugha nyingine si unajifunza tu ? .
 
Hivi kweli lugha ya kwanza iwe kihehe afu umudu standards za St Francis mbona hiyo kamba[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hata kama ni kikurya, ndiyo asiwe na mpangilio wa herufi, nukta na koma !!. Huyo huyo adai amesomea St Francis ?!.

Huyo demu tapeli.
 
Hata kama ni kikurya, ndiyo asiwe na mpangilio wa herufi, nukta na koma !!. Huyo huyo adai amesomea St Francis ?!.

Huyo demu tapeli.
Na anaweza asiwe ni demu hata ...unakuta ni limwamba fulani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚....Sema kama ni St Alumni kweli basi naanza kupata mashaka na one zao za single digits
 
Kweli usome St Francis usijue uandishi wa sentensi ?!. Huna cha herufi kubwa, koma wala nukta !!. Halafu lugha upate 'A'

Acha kutafuta misifa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapo kwa Consolata panaweza pakawa kamba ili kulazimisha hoja sema nn mm nimekupata hivyo hivyo
Wakiendaga advance shule za serikali hasa special wanakuaga weupeee. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hawana maajabu.
 
Na anaweza asiwe ni demu hata ...unakuta ni limwamba fulani [emoji23][emoji23][emoji23]....Sema kama ni St Alumni kweli basi naanza kupata mashaka na one zao za single digits
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
NAKAZIA!!!
Shule bora ni ile inayomfanya mwanafunzi kutoka F kwenda D,C,B au A na sio kama hao St.Francis na shule nyingine za binafsi ambazo zinafanya interview kuchukua wanafunzi ambao tayari ni wazuri.Kwa hapo tusifie wanafunzi na sio shule.
NAKAZIA TENA!!!!!
Siku hizi elimu imerahisishwa sana!!! tena mwaka huu.Eti sisi pale Marian Boys tuna div1.7 tisini na moja na watu wenye A flat ni 7 na hakuna hata mmoja aliyeingia top 10 kitaifa hata shule haijaingia wakati mwaka jana tu div1.7 zilikua thelasini na ushee na A flat zilikua mbili ambapo moja iliingia top 10 boys na nyingine top 10 kitaifa na shule ikawa top 10 sasa jaribu kulinganisha ufaulu ndani ya mwaka mmoja.
Tunapoelekea hiyo div1.7 itapoteza thamani tutaanza kutazama A level au chuo
 
Sasa mbona wakati anahojiwa na mwananchi alisema hakutegemea kuingia top 10 ila mapenzi ya Mungu.Ama kweli huko alipo baba wa taifa anaona adui wa nne wa taifa ambaye ni unafki.
 
Ni ile hofu ya siku ya kutangazwa matokeo tu, nimekwambia toka kafika St Fransis mpaka anaondoka alikua anashika namba moja tu na kila mwaka St Francis inaingiza kumi bora hivyo tulijua lazima aingie na hata mock Kanda alikua wa kwanza. Mama yake alimuahidi kitu fulani akiingia kumi bora. Na kwenye familia yeye sio wa kwanza kuingia 10 bora, wapo waliomtangulia na walisoma shule za serikali. Mama yake alichukua zawadi ya mwanafunzi bora Udsm na wamemsomesha mpaka PHD. Niamini nakwambia Conso alikua anasomea 10 bora
Sasa mbona wakati anahojiwa na mwananchi alisema hakutegemea kuingia top 10 ila mapenzi ya Mungu.Ama kweli huko alipo baba wa taifa anaona adui wa nne wa taifa ambaye ni unafki.
 
Hilo la maswali ya practical lilikuwepo Sana, maana mwalimu alikua anapewa barua mwezi mmoja kabla ya kuandaa vitu na barua ya masaa 24 kabla na hiyo ndio inaweza kumsaidia mwalimu kubashir maswali na kuwasaidia watoto. Shule nyingi hata za serikali walimu huwasaidia watoto na ndio maana mwaka huu, serikali imefuta barua ya 24 hours, Sasa ni masaa matatu kabla. Mwalimu hawez kupata muda wa kuandaa na kuonana na watoto
 
Kuandika kwa usahihi ni changamoto kwako halafu bado unataka tuamini wewe ulifeli kwasababu hukununua mitihani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…