St george ya ethiopia yamtaka coutihno wa yanga kwa $70,000!!

St george ya ethiopia yamtaka coutihno wa yanga kwa $70,000!!

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Klabu ya St George ya Ethiopia, imetuma ombi la kumtaka Andrey Coutinho wa Yanga wakati kiungo huyo mshambuliaji raia wa Brazil akipiga hesabu za kupewa uraia wa Tanzania ili aichezee Taifa Stars.


St George ambayo ni timu ya zamani ya Kocha wa Rwanda, Milutin Sredojevic ‘Micho’, imetenga dola 70,000 ili imsajili Coutinho ili ifanye vizuri katika ligi kuu ya nchi hiyo.

Mmoja wa mabosi wa Yanga amesema, St George imetuma ombi la kumhitaji Coutinho na sasa viongozi wanamsubiri mchezaji huyo na Kocha Hans van Der Pluijm ili kufikia muafaka.

“Kuna uwezekano mkubwa Coutinho akaondoka Yanga kwani St George imetoa ofa ya dola 70,000, hata hivyo tumeshindwa kutoa uamuzi hadi mchezaji atakaporudi na kocha pia,” kilisema chanzo chetu.

Wakati huohuo, habari zinasema Coutinho ameuandikia barua uongozi wa Yanga akiomba asaidiwe kupata uraia wa Tanzania ili aichezee Taifa Stars kwani hana nafasi ya kuichezea Brazil.

“Inaonekana amefurahia maisha ya Tanzania, kwani ametuomba ikiwezekana tumsaidie kupata uraia wa Tanzania ili aweze kucheza Taifa Stars,” kilisema chanzo hicho.
 

Attachments

  • maximo+aanza+tizi+2.JPG
    maximo+aanza+tizi+2.JPG
    63.6 KB · Views: 254
  • COUTINHO+YANGA+SANA+BALL_2.jpg
    COUTINHO+YANGA+SANA+BALL_2.jpg
    51.3 KB · Views: 280
Kama kweli iyo ofa ipo auzwee tu hakuna tabuu

Maana daima mbele
 
Fasta Fasta..... tunashukuru kwa mchango wake
 
Auzwe tu. Wabrazil wengine watakuja wenyewe Yanga.
 
Hiyo sahau kwa viongozi wenye akili mgando wa Yanga..wako radhi aende bure mwisho wa mkataba au atoroke kuliko kuuzwa
 
nenda jembe hapa bongo ndio hivyo tena taa nyekundu imeshaanza kukuwakia.
 
hiyo ofa inatosha aende tu
 
Hiyo mihela inafaa kabisa kwa kumuuza coutinho vinginevyo anaweza kuondoka bure...
 
Uraia wa Tanzania haupatikani kirahisi hivyo Coutihno...

Aende zake tu huko Ethiopia bila shaka atalamba mpunga zaidi...
 
Back
Top Bottom