TANZIA Staa wa tamthilia ya Ertugrul, Artuk Bey afariki dunia

TANZIA Staa wa tamthilia ya Ertugrul, Artuk Bey afariki dunia

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
1,667
Reaction score
2,595
Muigizaji wa tamthilia pendwa zaidi kwa sasa ya Uturuki ya Ertugrul, bwana Ayberk Pekcan maarufu kama Artuk Bey amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 51.
7a351719016a4be90656f38a3b1eb87d


Ayberk ambaye amecheza kama, Artuk Bey kwenye tamthilia hiyo ya Ertugrul, amekuwa akisumbuliwa na kansa kwa miezi kadhaa. Familia ya muigizaji huyo imethibitisha kifo chake hapo jana siku ya Jumatatu Januari 24, 2022.

Nyota huyo amekuwa kipenzi cha mamilioni ya mashabiki ambao wanafuatilia tamthilia ya Ertugrul akiwa ni miongoni mwa wahusika wakuu.
Muigizaji huyo aliwahi kuandika maelezo mafupi kuhusiana na hali yake ya kiafya miezi michache iliyopita kabla ya kifo chake

”Wapendwa marafiki…. Mchakato ambao ulianza na daktari niliyeenda kumalalamikia kuhusu maumivu ya mgongo umefikia hatua hii leo. Nina saratani ya mapafu. Pia imeenea kwenye ini na adrenal glands. Kwa bahati mbaya, ugonjwa huu haukuonyesha dalili zozote katika hatua zake za awali. Usaidizi wangu mkubwa ni pamoja na familia yangu. Vile vile na marafiki zangu walio karibu… Nitajitahidi niwezavyo kurudisha afya yangu.”

Taarifa za kifo chake zimeleta mshtuko mkubwa nchini Uturuki huku waigizaji wenzake wakituma salamu zao za pole.
 
Apumzike kwa Amani Ayberk Pekcan
 
Back
Top Bottom