KERO Stahiki kandamizi kuhusu kupunguzwa kwa wafanyakazi wa mgodi wa Almasi wa Mwadui (Williamson Diamonds Limited)

KERO Stahiki kandamizi kuhusu kupunguzwa kwa wafanyakazi wa mgodi wa Almasi wa Mwadui (Williamson Diamonds Limited)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mnamo mwezi Agosti kuliibuka tetesi kwamba kutakuwa na kupunguzwa kwa wafanyakazi katika mgodi wa Williamson Diamonds Limited uliopo katika umiliki wa Petra Group kutokana na sababu za kushuka kwa bei ya almasi katika soko la dunia.

Hata hivyo baada ya vikao kufanyika pamoja na voingozi wa vyama vya wafanyakazi wa mgodini, uongozi wa mgodi ulitoa waraka wiki iliyopita ya tarehe 16 septemba 2024 kuelezea maamuzi yaliyofikiwa pamoja na stahiki watakazopata wafanyakazi wote watakaopunguzwa.

Kupunguzwa ni changamoto ya kawaida inayoweza kutokea lakini malalamiko yanayotolewa na wafanyakazi ni stahiki kandamizi na zisizo za haki kwa wafanyakazi hawa ambao watapunguzwa. Naambatanisha picha za waraka huo mtusaidie kupaza sauti kwa mamlaka husika (ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo mwezi Agosti Naibu Waziri Mkuu alitembelea mgodi huo na kutoa maelekezo mbalimbali ikiwemo kuzingatia stahiki za wafanyakazi endapo mgodi utafanya uamuzi wa kuwapunguza)

Soma Pia: Mara: Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu CATA MINING warejesha mgomo, walala ofisini wakisubiri mshahara

WhatsApp Image 2024-09-23 at 1.03.51 PM.jpeg
WhatsApp Image 2024-09-23 at 1.03.51 PM(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-09-23 at 1.03.51 PM(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-09-23 at 1.03.52 PM.jpeg
ili

Watu hawa wapate haki zao kama inavyostahili kwa mujibu wa Sheria ya Kazi na miongozo ya nchi.
 
Back
Top Bottom