staili hii ya ndoa inavyonichosha!!

mkonowapaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
1,492
Reaction score
768
haya tena wapendwa wa jf......habari za masiku teele!!

bwana nakaa nawaza sipati jibu.........la haraka!!maana ni miezi kadhaa kijana nimebahatika kupata kibarua cha mkoani...juu kabisa kaskazini magharibi

ofkoz chuo ckua navaa miwani ya mbao..nikapata binti.tukapendana...kamaliza nayeye kapata kazi nyanda za juu kusinii..

so kuonana apo ni ishu kweli kweli....nimejaribu kuona jinsi ya kumhamishia huku lakini inakua ngumu kutokana na nature y akazi yake na yangu pia..si watu wa kutulia sehemu 1

wapendwa..kwa iyo inamaana baada ya honeymoon kila mtu anakamata begi lake anarudi alipotokea?siamini

hebu nipeni experience zenu wenye distance mariages..nimeanza kuingiwa na waswas maana hata mhusika nae anachukulia poa tu....
 
Kiongozi kwa maisha ya sasa usiumize sana kichwa juu ya hilo. Ukiangalia kuna ongezeko kubwa la ndoa za hivyo. Hakuna kitu kibaya ilimradi wote mnajua majukumu na wajibu wenu katika ndoa. Asilimia ya watu wanaoishi mbali mbali na wenzi wao imeongezeka sana siku hizi kwa hiyo hutakuwa wa kwanza.

Cha msingi ni kudumisha mawasiliano tu hapo na kujiwekea malengo ya muda fulani kisha muanze kuishi pamoja. Kwasasa mnajenga maisha yenu yajayo kwa hiyo jipeni moyo na mumtangulize Mungu mtafanikiwa tu.
 
Tenganeni kwa muda ila ni muhimu kufikiri jinsi ya kuishi pamoja.ndoa za distance zina matatizo makubwa mwenyewe ni muhanga.msichukue muda mrefu hasa mkishapata mtoto.
 
Kwa nini wewe usihame na kumfuata huyo mchumba huko huko au nawe nature ya kazi yako ni ngumu?
 
anayeweza kuhama kati yenu ahame. ikishindikana kwa kipindi hiki kila mmoja asake kibarua mahali pengine, iwe ambapo kutawafanya muwe karibu
 
Ila hii kitu imekaa vibaya sana. Mie sipati picha inapotokea unawazia siku ya honeymoon yenu, wakati mnaishi kigoma na mtwara, si majariu makubwa sana haya! Jikaze utashinda mkuu
 
Muhimu wote wawili muwe waaminifu huko mlipo bila kusahau kwamba mmekua wana ndoa hivyo mna majukumu zaidi.

Pili mawasiliano yawe mazuri ili msije mkaDrift na hatimae fall apart.

Tafuteni namna ya kukutana mara kwa mara. . . maadam mpo ndani ya nchi moja jitahidini isiende miezi miwili bila kukutana.

Mkikutana muda wenu ufanyeni uwe unawahusu nyie zaidi ya mambo mengine.

Na huo wasiwasi ulio nao unless una sababu ya msingi upotezee.
 
pole mkuu hii kitu sikia kwa mwenzio ikikutokea ndo utajuwa ugumu wake mapenzi katika hili hayana uvumulivu tusidanganyane ndo maana kuna uhamisho wa mke kumfuata mume na inatambulika kiserikali,nature ya kazi zenu sasa ndo sijajuwa,ila suluhisho kwa sasa ndo uwe unajitahd muonane mara kwa mara
 
Ila hii kitu imekaa vibaya sana. Mie sipati picha inapotokea unawazia siku ya honeymoon yenu, wakati mnaishi kigoma na mtwara, si majariu makubwa sana haya! Jikaze utashinda mkuu

dah enzi za mwalim haya mambo hayakuwepo kbs..mama nakua hom kazi kuangalia familia
 
Kama haiwezekani kuhama, wakati mnavumilia hiyo hali, boresheni mahusiano yenu huku kila mmoja akitafuta kazi mpya kwenye mkoa alipo mwenzake.



Il Gambino.
 
mhh mmeanza safari yenu ni vibaya kwani pamoja na uaminifu sidhani kama imani mtakuwa nayo ya kutosha
 
Asikwambie mtu bwana mdogo hizi ndoa mume yupo Songea mke Arusha zina matatizo yake. Ndoa nzuri ni ile ambayo mpo pamoja au kama ni umbali ni ule ambao mmoja akimhitaji mwenzake anampata bila tabu. Kinyume na hapo jiandalie kuchakachuliwa tu mzigo wako huko. Dunia imekwisha hii. Tabu yote ya nn? Tafuta wa karibu yako.
 
Mimi mbona nilhama nikamfuata mke wangu???hayo maisha ya kukaa mbalimbali hayana maendeleo kabisa,jitahidi mmoja wenu atafute kazi karibu na mwingine..Inabidi pia mchague wapi makao yenu makuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…