IZENGOB
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 323
- 317
Mfumo huu ni umekua ni wa hovyo sijawahi kuona.Fikiria mkulima amejinyima kula vizuri,kuvaa na watoto wake lakini leo hii mkulima anakuja kumkopesha tajiri ambaye ana mali kedekede inauma sana.
Zaidi ya mwezi sasa tangu niuze mazao yangu kwa mfumo huu ambao serikali imeshindwa kuusimamia sijalipwa pesa yangu ya ufuta jambo ambalo linanipa wakati mgumu na maisha yangu kuendelea kuwa magumu kila kukicha.
Wanunuzi wa mazao haya ni matajiri wakubwa ambao wanatunyonya wakulima hali ambayo inatufanya wakulima kuendelea kuwa na maisha magumu.
Hebu fikiri
Hakuna pembejeo yoyote ya ambayo mkulima kapewa.Wala hakuna msaada wowote wa pesa wala kitaalamu ambao unatolewa kwa mkulima lakini mkulima amekuwa akikopwa mazao yake na wengine kudhulumiwa kabisa.
Kuna haja gani ya kuwa na mfumo huu katika nyakati hizi za sayansi na technolojia.Sisi wakulima tunaomba kuuza mazao hetu na pesa kupewa palepale au kuandikiwa cheki palepale.
Ni wazi kiwa wizara husika wanashindwa kuona kuwa sisi wakulima wa nchi hii tunadhurumika pakubwa.Mh Bashe Huoni kuwa wizara yako inashindwa kusimamia vyema makampuni yanayonunua mazao kutoka kwa wakulima? Sioni sababu ya kuwa na mfumo huu kandamizi na onevu kwa mkulima.