STAMICO watoa gawio. Nao wamekopa?

STAMICO watoa gawio. Nao wamekopa?

Nasikia wame sign mkataba WA kuvuna Makaa ya mawe Kwa Tani tzs 69,000/- Ilihali kwenye soko ni tzs 240,000/- Hilo gawio ni dhihaka
 
Leo STAMICO wametoa gawio la 2.2 B kwa serikali.

Juzi Mama yenu alikuwa anaponda Mashirika kuwa yalikuwa yanakopa ili kutoa gawio kwa Serikali.

Sasa naona na yeye anaenda mulemule.

Kukaa na mnafiki ni hatari kwa afya na maisha yako.
Jiulize kwanza STAMICO inafanya biashara gani.
 
Stamico wanamiliki Mgodi pale stamigold aka the old tulawaka. Stamigold wana kazi wanazifanya migodini kama pale GGM nk.

Kifupu ni taasisi ambayo kiasi fulani inapaswa kutoa hela aka gawio, sisemi wengine wasitoe gawio lakini kuna mashirika mengine unayaona kabisa yanayumba kiasi kwamba yenyewe yanahitaji mtaji lakini maajabu ya Mussa eti yanatoa gawio halafu siku chache unaonao au kusikia wamepata hasara.
 
Leo STAMICO wametoa gawio la 2.2 B kwa serikali.

Juzi Mama yenu alikuwa anaponda Mashirika kuwa yalikuwa yanakopa ili kutoa gawio kwa Serikali.

Sasa naona na yeye anaenda mulemule.

Kukaa na mnafiki ni hatari kwa afya na maisha yako.
Watetezi wa mwenda _zake mnapata taabu Sana...
 
Tunawasubiri hawa ATCL na TTCL wagawa gawio maarufu enzi za awamu 5 siku yao ya kugawa
 
Cde Samia naone Ile kauli, ilimtoka tu sio kama alikusudia. Kama kweli bodi zilikuwa zinakopa kwenye mabenki harafu mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali katika ukaguzi wake asizione, ila azione hela za tamisemi zilizokwenda kwenye halmashauri zetu kwa ajili ya saruji za vituo vya afya. Hivi kweli inaingia akilini mabilioni ya mkopo benki yasionekane kwenye hesabu za mkaguzi wa serikali kisha vijisent iliyoibwa kwa ajili ya saruji. Vionekane kwa mkaguzi. Kama ni kweli cde Samia umetukisea sana kumbakisha kwenye ofisi ya umma mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali. Maana toka aanze ukaguzi hatukuwa wayi kusikia kama menejimenti pamoja na bosi za mashirika ya umma walikuwa wakikopa mikopo ya ovyo pasipo kufata taratibu.
 
Back
Top Bottom