Cde Samia naone Ile kauli, ilimtoka tu sio kama alikusudia. Kama kweli bodi zilikuwa zinakopa kwenye mabenki harafu mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali katika ukaguzi wake asizione, ila azione hela za tamisemi zilizokwenda kwenye halmashauri zetu kwa ajili ya saruji za vituo vya afya. Hivi kweli inaingia akilini mabilioni ya mkopo benki yasionekane kwenye hesabu za mkaguzi wa serikali kisha vijisent iliyoibwa kwa ajili ya saruji. Vionekane kwa mkaguzi. Kama ni kweli cde Samia umetukisea sana kumbakisha kwenye ofisi ya umma mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali. Maana toka aanze ukaguzi hatukuwa wayi kusikia kama menejimenti pamoja na bosi za mashirika ya umma walikuwa wakikopa mikopo ya ovyo pasipo kufata taratibu.