Stamina na mistari ya kuunga-unga

"Zaidi kuwataja kina Geez,Babuu,Kala,na Mansulii kuwa wasanii bora wa hiphop,tena kwa miaka 10 ijayo imedhihirisha wewe ni mbumbumbu wa hiphop!Hata FidQ na Jmoe hawawezi freestyling,nguzo muhimu ya kuwa MC wa ukweli"

hapa ndio ambapo nakuunga mkono kwa 50% then 50% yangu nyingine nabaki nayo,

50% hii chukua ya kuwa na mshangao wa kama mimi kwa wasanii kama babuu wa kitaa, geez mabovu, kala na mansuli kuwekwa kwenye wasanii bora,
nadhani mapenzi binafsi yamemgusa mtoa thread, maana hao aliowataja ukiwasimamisha na hiki kizazi cha watoto wa juzi kina one the incredible, nick mbishi n.k hawawezi kugusa moto wao,

50% ambayo nabaki nayo ni ya wewe kupinga fid q na jmo wasiwe best hiphop kisa hawajui freestyle, nadhani kaka hapa umepitiwa kidogo,
labda cjui freestyle gani ambayo unaisema wewe,

unapotaja 10 bora ya hiphop artist hauwezi ukaacha haya majina, hata ukipewa 5 bora bado yatakuwepo.
 

punguza mahaba coz yanadhoofisha uwezo wako wa kufikri........hata siku moja hatutumii filings kufikiri
 
nakubaliana na ww 60%!! ngoma ya stamina mpya na fid q cjaona ki2 cha maana sana zaid ya mistari yake hiyo ya kiujanja ujanja 2 mfano-(taifa linaitaji sensa ya mateja) (unakula unga utafikiri unaundugu na bakhresa) mistari ya kiwaki sna kwa mc wa hip hop!! ukija kwa roma mkatoliki hii track yake nilipoisikiliza ni taarifa ya habari baada ya kupata kilichafata nikaidelete 2 haina mzuka kabxaa yan kama unasomewa gazeti, atafute mambo mengne yakuongelea sasa. ni hayo 2*
ila iyo list yako ya wasanii umechemshaa
 

pamoja kaka coment yako ya maana sana....ebu weka list ya wasanii wako bora wa hip hop bongo
 
coment yako nzuzri sana but imepungukiwa kitu hivi,,,,,hebu taja basi wasanii wako bora was hip hop bingo
 

Ngoja nichukue na 50% uliyobaki nayo.
Kumbuka mleta uzi katumia maneno '...kwa miaka 10 ijayo'.hapo ndipo hatuwezi sema kwa hakika kina Fid na Jmoe WATAENDELEA kuwa miongoni mwa wasanii bora wa hiphop,kwa kukosa hiyo element ya uwezo wa kufreestyle niliyoizungumzia.kuna watoto wapo jikoni wanapikwa kumaster freestlying,hvyo wakistick kwenye game rules ndani ya hyo miaka 10 itakuwa ni stori nyingine.
Freestlye ni uwezo wa kunata kwa vina vya papo kwa papo vyenye maana kwa aina yoyote ya mada utakayopewa kuizungumzia.MCs wa ukweli lazima uwe na huo uwezo,sio tu kuandika rhymes na kukariri kutengeneza track.
 
punguza mahaba coz yanadhoofisha uwezo wako wa kufikri........hata siku moja hatutumii filings kufikiri

'filings' sijajua ndo makitu gani.
Ila nachojua 'feelings' zinatokana na senses za binadamu na zina influence kubwa katika kufikiri kwake.
Ni vema ungejibu hoja kwa hoja,ama hukutaka kupingwa mkuu?haya basi umepatia.
 
mimi uwa nabaki nashangaa wanaodai wanajua hip hop, kila mtu anajifanya anaijua hip hop zaidi ya mwenzake.
Utasikia huyu anadai mwana hip hop anatoa misingi yake.
Huyu anakuja anasema yule haimbi hip hop ana rap tu.
Sasa mimi sielewi elewi nani anaimba hip hop
 

Nilipoweka rangi ya Blue umeandika point,but nilipotupia wino mwekundu umeandika pumba mshkaji wangu.Hakuna hata mmoja hapo anayestahili hata 20 bora
 
Prof J! Malizia lakini muziki wa leo lazima msanii atapaje shows naakipata atawarushaje mashabiki!
 
1.Prof.Jay. 2.Jay Mo. 3.Fid Q. 4.Joh Makini. 5.Ulamaa a.k.a Msafiri. 6.Mwana FA. 7.Nash MC (Up coming). 8.One the Incredible. 9.Kala Jeremiah (just expectation) .10.Stamina
 
Muziki unabadilika na wakati (transformation katika Hip Hop Ipo) Hata uko marekan ilipoanza hip hop sidhan nicky minaj na wenzake wanaimba HIP HOP zile za miaka ile , unasema stamina anafanya ujanjaujanja kafanye wewe tukuone kama UTAKUA JUU , ROMA anaunganisha vichwa vya habar kaunganishe wewe tuone kama utatoka, WASANII ULIOWATAKA HAPO MBONA NAO WAKAWAIDA SANA MABOVU, BABUU WA KITAA wanaimba nini hao , hip hop imebadilika tena sana sasa wewe unataka watu waimbe hip hop ya miaka ya tisini wakati kizaz cha 2013 hakiitaj hizo hip hop za tisini, SASA KAMCHUKUE HUYO MABOVU, MANSULI, Babuu Wa Kitaa Waandalie Shoo Uone Kama Ukumbi Watajaza, Hafu Wachuke Hawa Kina Stamina,roma Waandalie Shoo Uone Watu Watakao Jaza Mwisho Ndo Utapata Jibu Wasanii Wag Wanawaeeleweka na HIP HOP ZAO KWA MASHABIKI , Hip Hop Ni Uhalisia Imba Vitu Vinavyotoke Kwenye Jamii Na Kuwagusa Watu Moja Kwa Moja ndo maana roma anaendelea kupendwa hata kama wewe usipomkubal sio lazima kwan we nan
 
stamina hafuati lyrical concept of mcee nashangaa mnavosema ni mkali 'mfupi ndo mtu aliyegundua ngazi apate vya juu' ina maana kweli?!,kinachomueka ni #PROMO
 
mziki wa bongo umejaa fitina ndio maana emcee wakali waliacha game nakufanya mambo yao ya msingi hv kuna emcee anaye mfunika hashim dogo au zavara au salu T mtaje ?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…