Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!

Kamongo

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2009
Posts
2,190
Reaction score
2,485
Nafikiri watu wengi mnakumbuka yule mwandishi wa habari miaka ya themanini na tisini marehemu stan Katabaro,alikuwa ni mwandishi mahiri kwa miaka ya leo hana tofauti na Saed Kubenea,Johnson Mbwambo,nauliza kifo chake kilisababishwa na nini hasa?wanaokumbuka watujuze

 
Alikufa ghafla!

Kumfananisha Kubenea na Stan, ni kumpandisha tuu chati Kubenea, Stan alikuwa akiandika investigative journalism kwenye developing story, Kubenea anaandika udaku kwenye medani za siasa, sio uchunguzi in a really sense ya uchuguzi.

Waliotaka kufuata nyanyo za Katabalo, ni This Day na Kulikoni, walioanza, wakati wakifuatilia story ya Rada.
 
Masikini_Jeuri

Gazeti lake liliitwa Mfanyakazi, kila wiki nilihakikisha napata nakala yangu. Humo ndani pia kulikuwa na hadithi za mtunzi maarufu Agoro Anduru, sijui kaishia wapi siku hizi. Na column fulani ndogo ya vichekesho iliyokuwa ikiitwa Nipashe, yenye picha ya sikio kuubwa.

Nilisikitishwa sana na kifo cha Stan Katabaro, Mungu amweke pema na aisaidie familia yake, Amen.
 
Last edited by a moderator:
ni kweli kabisa pasco...

Tatizo kubwa la kubenea ni ku-personalize uandishi wake na hivyo kuwa na agenda moja tu,
 
Siamini sana uchawi lakini kifo chake kinasemekana kulikuwa na mkono wa mtu.

Aliwasumbua sana jamaa na kashfa ya Loliondo na mpaka walitishia kumuua lakini hakuacha kuandika. Tulikuja kushtukia amekufa tayari lakini alikuwa ni mwandishi mahari ambaye akianza kuriporti tukio ni mwanzo mpaka mwisho. Lakini Ndolanga (mkurugenzi wa wanyama pori wakati ule na Rais Mstaafu Mwinyi) wanaweza kueleza kilichomkuta!!! Inawezekana alilishwa sumu bila kujua.

RIP Stan Katabaro. Hivi alikufa na gazeti lake la mfanyakazi? Mbona silioni wala kulisikia siku hizi?

Tiba
 
Hawezikulinganishwa na waandishi uchwala wa sasa huyu bwana alikuwa na team nyingine ya madongo.

Mnamkumbuka Stanley KAMANA wa Family Mirror (RIP) hawa wote walikufa vifo vya ajabu ila ikumbukwe pia wakati hule lile janga la UKIMWI lilikuwa halijulikani na mtu aliyeugua dalili zake zilikuwa zinaelekezwa kwa Prof. Maji Marefu naye hakuwa na hiyana ya kubadilisha kibao mpaka pale walipomshutukia na kumfukuza Dar ila alichafua hali ya hewa mitaa ya Kariakoo na Ilala.
 

Agoro Anduru (The Temptation) ni Marehemu pia (RIP)

Stan hawezi kulinganishwa na mwandishi yeyote katika hii decade 2000 - 2010! Kubenea, Mbwambo, e.t.c they are no where near - kumbuka kuwa wakati the so called "uhuru wa vyombo vya habari" ulikuwa mdogo sana!

RIP Stan K.
 
Hawa ndo walikuwa waandishi bwana, ila Kubenea naye namkubali, Mnamkumbuka Kabendera Shinani? Naye aliuwawa kule BK kwa kina IWE na alikutwa anaelea ziwani. Wanasema naye alikuwa akifuatilia kashafa moja ya utekaji wa magari mkoani Kagera ambapo kigogo mmoja huko mkoani alikuwa anahusika!
 
Gazeti lake liliitwa Mfanyakazi, kila wiki nilihakikisha napata nakala yangu. Humo ndani pia kulikuwa na hadithi za mtunzi maarufu Agoro Anduru, sijui kaishia wapi siku hizi.

Ulipomtaja marehemu Agoro Anduru umenikumbusha vipaji vya uandishi wa huyu mwana riwaya mahiri.............jamani walikuwepo watanzania wenye vipaji ambao taifa hili halitaki hata kuwaenzi............Sijui kwa nini....
 

Kama kawaida yako mzee unajiamini sana na unaweza kusema lolote lile. Kumbuka kuwa hata KGB ilisambaratika!
 
Je, mnakumbuka na ile kashfa ya RIO? Kwenye mkutano wa Mazingira Duniani ulifanyika BRAZIL (Rio de Janeiro)

Kwahakika hakuna kama STAN KATABALO.

Kashfa ya LOLIONDO ilimhusu sana sana ABUBAKAR MGUMIA......

Huyo bwana ndiye aliyekuwa mhimiri wa kashfa ya Loliondo kabla ya kutolewa Wizara ya Utalii na kupelekwa kuwa RC Singida. Hivi siku hizi yuko wapi huyo Mgumia?


RIP Katabaro.....Namkumbuka sana jinsi alivyokuwa mwandishi mzuri sana na asiye na woga.

Wadau naomba pia mkumbuke jamaa mmoja anaitwa Anthony Ngaiza ambaye aliwahi kuwa editor wa Family Mirror kwenye miaka ya 1992/93 kabla ya kuhamia MCT. Tunahitaji kweli kuwakumbuka hawa jamaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…