Stanbakora, Mkude Simba, Bwakila, Kitale: Nani ni nani?

Hahaha hawa hunifanya niisikilize E-FM
Wanastahili pongezi kwa njia ile maana E FM wasingeweza kupenya kwenye tasnia hii,

kama ni Muziki kila radio inajitahidi kupiga Muziki mzuri hata Uhuru wanapiga mziki mzuri ila hawana wasikilizaji kabisa ingawa mi sisikilizagi ila nikikumbuka mwanzoni E FM wanaaanza walikuwa wanaweka vichekesho kila baada ya kupiga nyimbo kadhaa kwahio sisi wasikilizaji tukawa tunatega sikio kuwasikiliza hawa jamaa tu.
 
Redio uhuru sisi wazee wazamani, siku za j.mosi saa 3:30 usiku kuna muziki mzuri wa kitanzania, mziki wa miaka ya 80 mpaka 90 enzi ya band za legho, uda, DDC mlimani park, bima, tancurt, urafiki, washirika, Mk group, OSS, Juwata, maquis, mwenge jazz. Na band nyingi za wakati huo mziki wake husikika hapa, Alhamis RFA saa 4:00 usiku j.pili E. FM mimi sina mapenzi na Radio nina mapenzi na vipindi nasikitika Radio One sijui wamefanyaje siwapati vizuri kwenye radio ingawa wapo.
 
Radio one kuanzia jumatatu had alihamis saa nne usiku ni ngoma za zamani tu..... Wametufukuza sisi wapenz wa chombeza time,,, maana mziki wa chombeza time ni mzito hamna radio ingine inapiga mziki huo

Radio one hawajatutendea haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…