Stand ya Nanenane Dodoma ukipaki gari unapoingia kwa abiria unalipishwa, hata kama una tiketi ya basi

Stand ya Nanenane Dodoma ukipaki gari unapoingia kwa abiria unalipishwa, hata kama una tiketi ya basi

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Nimepita stand ya Nanenane Dodoma leo, kuna kitu sijakielewa.

1. Ukiingia na gari, wanakulipisha ushuru wa kuingia na gari na wanakupa tiket.

2. Ukipaki gari, unapoingia kwa abiria unalipishwa, hata kama una tiket ya bus. sasa mimi kwa mfano, nimekuja na mwanafamilia nikiendesha gari yangu, nafika getini nalipa na kupewa tiket, kwasababu nasafiri namwachia dogo gari airudishe home, kuingia kwa abiria nalipishwa tena, wakati mkononi nina tiketi ya gari niliyokuja nayo na tiketi ya basi ninalosafiri nalo, unanilipishaje sasa?

HOJA; sijaona hoja ya msingi kwanini nikiwa tayari nina tiketi nilipishwe tena kuingia kwa abiria wakati stand yenyewe imejengwa kwa pesa zetu sisi walipakodi. hiyo hela wanakata kwa kuingia tu (hata kama nina tiketi) inaelekea wapi? au inaenda hazina, au halmashauri, au wapi? Kufanyia nini?

Ingekuwa stand haijaboreshwa tungesema wanataka kuboreshea stand, ila tayari imeshajengwa na mle ndani wanachukua kodi kwa wapangaji na kwa magasi yote yanayoingia usiku na mchana na hadi vyoo walalipisha, sasa mimi abiria ambaye nilishakata tiket naenda tu pale kupanda basi wanakata hela yangu kwa justifications gani? Au stand zote zipo hivyo? Hela wanayokata ni ndogo lakini nachelea kusema kwamba kuna raia wa hali ya chini wanaweza kuona ni mzigo, tulidhani hii stand imejengwa kwa pesa zetu itumike kama huduma/service. isijekuwa wanakata pesa zetu hizo wanatia mfukoni, mwenye kujua hili atufafanulie.
 
Nimepita stand ya Nanenane Dodoma leo, kuna kitu sijakielewa.

1. ukiingia na gari, wanakulipisha ushuru wa kuingia na gari. na wanakupa tiket.

2. ukipaki gari, unapoingia kwa abiria unalipishwa, hata kama una tiket ya bus. sasa mimi kwa mfano, nimekuja na mwanafamilia nikiendesha gari yangu, nafika getini nalipa na kupewa tiket, kwasababu nasafiri namwachia dogo gari airudishe home, kuingia kwa abiria nalipishwa tena, wakati mkononi nina tiketi ya gari niliyokuja nayo na tiketi ya basi ninalosafiri nalo, unanilipishaje sasa?

HOJA; sijaona hoja ya msingi kwanini nikiwa tayari nina tiketi nilipishwe tena kuingia kwa abiria wakati stand yenyewe imejengwa kwa pesa zetu sisi walipakodi. hiyo hela wanakata kwa kuingia tu (hata kama nina tiketi) inaelekea wapi? au inaenda hazina, au halmashauri, au wapi? kufanyia nini? ingekuwa stand haijaboreshwa tungesema wanataka kuboreshea stand, ila tayari imeshajengwa na mle ndani wanachukua kodi kwa wapangaji na kwa magasi yote yanayoingia usiku na mchana na hadi vyoo walalipisha, sasa mimi abiria ambaye nilishakata tiket naenda tu pale kupanda basi wanakata hela yangu kwa justifications gani? au stand zote zipo hivyo? hela wanayokata ni ndogo lakini nachelea kusema kwamba kuna raia wa hali ya chini wanaweza kuona ni mzigo, tulidhani hii stand imejengwa kwa pesa zetu itumike kama huduma/service. isijekuwa wanakata pesa zetu hizo wanatia mfukoni, mwenye kujua hili atufafanulie.
Kama wezi CCM hawajaichukua na kudai yao mnabahati kwelikweli tena kweli.
 
2. ukipaki gari, unapoingia kwa abiria unalipishwa, hata kama una tiket ya bus. sasa mimi kwa mfano, nimekuja na mwanafamilia nikiendesha gari yangu, nafika getini nalipa na kupewa tiket, kwasababu nasafiri namwachia dogo gari airudishe home, kuingia kwa abiria nalipishwa tena, wakati mkononi nina tiketi ya gari niliyokuja nayo na tiketi ya basi ninalosafiri nalo, unanilipishaje sasa?
Ukisikia economic rapping ndiyo hiyo ipo Mbezi pia
 
Kwa ajili ya uendeshaji wa stendi kama umeme, ulinzi, usafi nk

Pia kama wame kulipisha mara mbili hilo ni tatizo lakini mimi haijawai tokea, ina tokea pale ambapo sina tiketi ya basi na nimeshuka kwenye basi
 
Hivi Magufuli Stand napo walipisha hivyo vifurushi?
 
Kama utakua hujaongeza chumvi basi watakua wamekupiga tu..me nilienda hapo nikiwa na ticket mtandao ya shabiby na niliingia bila shida yoyote.
 
Kituko ni kwamba LATRA wana hamasisha E- tickets lakini ukiwaonesha SUMA-JKT pale getini hawaitambui wanataka uwe na hard copy.
Utalipishwa tu.
Hii sio kweli kabisa,juzi tu hapa nimetoka kusafiri na nilikua na ticket mtandao na hakuna suma jkt aliyenisumbua,tena ukifika pale getini wanasema kabisa kama una ticket ya mtandaoni pita huku wakiwa na maana kuna sehemu unapita ambapo kuna mlinzi kazi yake ni kuzikagua hizo ticket mtandao.
 
Basi wamebadilika au uliye kutana nae.
Mimi sijawahi toboa na tiketi ikiwa kwa mfumo wa SMS.
 
Lipa kodi kwa maendeleo yako
Sh 200 hio ndio inalipq vitu vyote matv mle mavingamuz usafi maji.changia kwa uzalendo.si risit unapewa,jua impo mikono salama
 
Back
Top Bottom