Stand ya Nanenane Dodoma ukipaki gari unapoingia kwa abiria unalipishwa, hata kama una tiketi ya basi

Tanzania linajengwa daraja kwa pesa za walipa kodi watu wanampongeza sana kiongozi likishaisha kuvuka daraja wanachajiwa kulipia ili kuvuka daraja Nchi hii kiboko aisee ina watu wakatili sana wakiweka ujambazi mbele wanaamua kufanya chochote tu ili mradi wao wapate..
 
Hata mimi nilishangazwa kutakiwa kulipia pesa wakati ninayo tiketi hapo nane nane stendi. Tena wameweka na tangazo kabisa. Ule ni uwizi wa mchana.
 
Unashangaa hiyo wanalipisha tiketi hadi kutoka wale SUMA JKT wana njaa sana.
tunahitaji kujua nafikiri wapi hizo pesa zinaenda, kama zinaenda kwenye kapu la taifa sawa, isije kuwa zinaenda kwa mkurugenzi au kwa watu fulani. na kama zinaenda kwa ndugu zetu walinzi wa SUMAJKT tujue ili tuwe na moyo huru kusaidia hao ndugu zetu.
 
Nimepita stand ya Nanenane Dodoma leo, kuna kitu sijakielewa.

1. Ukiingia na gari, wanakulipisha ushuru wa kuingia na gari na wanakupa tiket.

2. Ukipaki gari, unapoingia kwa abiria unalipishwa, hata kama una tiket ya bus. sasa mimi kwa mfano, nimekuja na mwanafamilia nikiendesha gari yangu, nafika getini nalipa na kupewa tiket, kwasababu nasafiri namwachia dogo gari airudishe home, kuingia kwa abiria nalipishwa tena, wakati mkononi nina tiketi ya gari niliyokuja nayo na tiketi ya basi ninalosafiri nalo, unanilipishaje sasa?

HOJA; sijaona hoja ya msingi kwanini nikiwa tayari nina tiketi nilipishwe tena kuingia kwa abiria wakati stand yenyewe imejengwa kwa pesa zetu sisi walipakodi. hiyo hela wanakata kwa kuingia tu (hata kama nina tiketi) inaelekea wapi? au inaenda hazina, au halmashauri, au wapi? Kufanyia nini?

Ingekuwa stand haijaboreshwa tungesema wanataka kuboreshea stand, ila tayari imeshajengwa na mle ndani wanachukua kodi kwa wapangaji na kwa magasi yote yanayoingia usiku na mchana na hadi vyoo walalipisha, sasa mimi abiria ambaye nilishakata tiket naenda tu pale kupanda basi wanakata hela yangu kwa justifications gani? Au stand zote zipo hivyo? Hela wanayokata ni ndogo lakini nachelea kusema kwamba kuna raia wa hali ya chini wanaweza kuona ni mzigo, tulidhani hii stand imejengwa kwa pesa zetu itumike kama huduma/service. isijekuwa wanakata pesa zetu hizo wanatia mfukoni, mwenye kujua hili atufafanulie.
u[po sahihi mkuu
 
Kwa ajili ya uendeshaji wa stendi kama umeme, ulinzi, usafi nk

Pia kama wame kulipisha mara mbili hilo ni tatizo lakini mimi haijawai tokea, ina tokea pale ambapo sina tiketi ya basi na nimeshuka kwenye basi
pale kuna maduka mengi tu mmekodisha, mabasi yote yanayoingia pale yanalipa pesa nyingi tu, ni umeme gani huo mnatumia, usafi gani huo kuhitaji hadi mchukue hela ya mlalahoi kiasi hiki? kwa siku pale mbezi au nanenane dodoma mabasi mamia yanaingia na sidhani kama yanaingia bure, kweli haitoshi kulipia umeme, usafi n.k? kwanini ccm huwa mnatafuta sababu tuwaite wezi? mnaumiza raia wa chini.
 
Nimepita stand ya Nanenane Dodoma leo, kuna kitu sijakielewa.

1. Ukiingia na gari, wanakulipisha ushuru wa kuingia na gari na wanakupa tiket.

2. Ukipaki gari, unapoingia kwa abiria unalipishwa, hata kama una tiket ya bus. sasa mimi kwa mfano, nimekuja na mwanafamilia nikiendesha gari yangu, nafika getini nalipa na kupewa tiket, kwasababu nasafiri namwachia dogo gari airudishe home, kuingia kwa abiria nalipishwa tena, wakati mkononi nina tiketi ya gari niliyokuja nayo na tiketi ya basi ninalosafiri nalo, unanilipishaje sasa?

HOJA; sijaona hoja ya msingi kwanini nikiwa tayari nina tiketi nilipishwe tena kuingia kwa abiria wakati stand yenyewe imejengwa kwa pesa zetu sisi walipakodi. hiyo hela wanakata kwa kuingia tu (hata kama nina tiketi) inaelekea wapi? au inaenda hazina, au halmashauri, au wapi? Kufanyia nini?

Ingekuwa stand haijaboreshwa tungesema wanataka kuboreshea stand, ila tayari imeshajengwa na mle ndani wanachukua kodi kwa wapangaji na kwa magasi yote yanayoingia usiku na mchana na hadi vyoo walalipisha, sasa mimi abiria ambaye nilishakata tiket naenda tu pale kupanda basi wanakata hela yangu kwa justifications gani? Au stand zote zipo hivyo? Hela wanayokata ni ndogo lakini nachelea kusema kwamba kuna raia wa hali ya chini wanaweza kuona ni mzigo, tulidhani hii stand imejengwa kwa pesa zetu itumike kama huduma/service. isijekuwa wanakata pesa zetu hizo wanatia mfukoni, mwenye kujua hili atufafanulie.

Na ukiingia chooni unalipishwa tena [emoji23].. wakati Airport msalani unaingia free tu
 
Back
Top Bottom