Stand ya Nanenane Dodoma ukipaki gari unapoingia kwa abiria unalipishwa, hata kama una tiketi ya basi

Tanzania linajengwa daraja kwa pesa za walipa kodi watu wanampongeza sana kiongozi likishaisha kuvuka daraja wanachajiwa kulipia ili kuvuka daraja Nchi hii kiboko aisee ina watu wakatili sana wakiweka ujambazi mbele wanaamua kufanya chochote tu ili mradi wao wapate..
 
Hata mimi nilishangazwa kutakiwa kulipia pesa wakati ninayo tiketi hapo nane nane stendi. Tena wameweka na tangazo kabisa. Ule ni uwizi wa mchana.
 
Unashangaa hiyo wanalipisha tiketi hadi kutoka wale SUMA JKT wana njaa sana.
tunahitaji kujua nafikiri wapi hizo pesa zinaenda, kama zinaenda kwenye kapu la taifa sawa, isije kuwa zinaenda kwa mkurugenzi au kwa watu fulani. na kama zinaenda kwa ndugu zetu walinzi wa SUMAJKT tujue ili tuwe na moyo huru kusaidia hao ndugu zetu.
 
u[po sahihi mkuu
 
Kwa ajili ya uendeshaji wa stendi kama umeme, ulinzi, usafi nk

Pia kama wame kulipisha mara mbili hilo ni tatizo lakini mimi haijawai tokea, ina tokea pale ambapo sina tiketi ya basi na nimeshuka kwenye basi
pale kuna maduka mengi tu mmekodisha, mabasi yote yanayoingia pale yanalipa pesa nyingi tu, ni umeme gani huo mnatumia, usafi gani huo kuhitaji hadi mchukue hela ya mlalahoi kiasi hiki? kwa siku pale mbezi au nanenane dodoma mabasi mamia yanaingia na sidhani kama yanaingia bure, kweli haitoshi kulipia umeme, usafi n.k? kwanini ccm huwa mnatafuta sababu tuwaite wezi? mnaumiza raia wa chini.
 

Na ukiingia chooni unalipishwa tena [emoji23].. wakati Airport msalani unaingia free tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…