Stanslaus Mabula aliwa kichwa Nyamagana, umekula na wewe umeliwa!

jindundu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
679
Reaction score
581
Ma CCM yamemla kichwa Mabula na kupeleka jina la Nzilanyingi kugombea Ubunge kwenye Jimbo hilo.

Japokuwa watu wanaimba kama kasuku, Uchaguzi haupo utadhani kuimba huko kutawazuia watu mjini na vijijini kwenda kupiga kura, lakini binafsi nimefurahi jamaa kuangukia pua

Siku ya Uchaguzi wa kura za maoni ndani ya Chama hicho Ubunge na Udiwani katika Kata zote za Jimbo hilo, nzi wangu.mzoefu akiwa amefungwa Camera alifanikiwa kujipenyeza kwa Siri na kushuhudia makuwadi au machawa wa Mbunge huyo wa zamani wakitoa rushwa kwa wajumbe kama njugu.

Lengo la kumtuma nzi wangu kufuatilia upigaji wa kura za maoni za Ubunge na Udiwani Jimbo hilo, lilikuwa ni kutaka kujionea kwa macho jinsi rushwa livyokuwa imeshamiri kwenye mchakato huo.

Katika Kata ya Luchelele, Kwenye Kituo cha kupigia kura cha Shule ya Sekondari Nsumba, machawa wa Mabula waliokuwa wakisambaza rushwa kwa Wajumbe ni Katibu Mwenezi wa UVCCM Kata hiyo ambaye aliongozana na Mwalimu wa Shule hiyo aliyejulikana kwa jina Moja la Machibya. Walizunguka.kwa wajumbe kwa kutumia pikipiki iliyoandikwa SSH. Kifupi cha Samia Suluhu Hassani.

Kutumia pikipiki yenye nembo ya jina la Samia Suluhu Hassan kugawa pesa ni kama walimwakilisha Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, kutoa rushwa bila kificho.

Kudos, Mabula kaliwa kichwa! Pesa siyo kila kitu, unaweza kutumia pesa kwa malengo ya kula pesa, lakini watu wakala pesa na usipate pesa uliyotegemea kula kutokana na wewe kutoa pesa!!!

Naelekea porini kwenye matambiko ya wazee!
 
Mmh ccm haina mwenyewe.
 
Back
Top Bottom