Starehe za Mlimani City na bei za ajabu ajabu

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
14,834
Reaction score
32,522
Hivi wakuu nyie mnawezaje kumudu bei za pale kuanzia vyakula mpaka vinywaji?

Kuna siku nimeuziwa glass ya juice ya pineapple 5000, mpka nikajicheka, nikauliza popcorn za chumvi eti 4000..wale watu sidhani kama wapo serious.

Imefika muda nikienda yale maeneo nakuwa mzito kutumia visenti vyangu, hivi nyie mnaokula pizza, bugger na kulewa pale samaki samaki mnaweza vipi? Au mnajitoa akili tu?
 
KUNA SEHEMU UKITEMBELEA UTASEMA NI NJE YA TANZANIA...
 

Hicho ndiyo Kijiwe Kikubwa na Makao Makuu ya Kupumzika ( Kula Bata ) na Kupanga Mikakati zaidi kwa Wauza Dawa za Kulevya wengi nchini Tanzania , Matapeli wakubwa nchini na Mafisadi pamoja na Wala Rusha wakubwa pia. Kama ulikuwa hulijui hilo pole mno Mkuu na natumai kwamba kuanzia leo utakuwa umeshapata Jibu lako. Fanya Utafiti wako juu ya haya niliyokuambia na najua ipo Siku utakuja Kukubaliana nami hapa hapa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Siku ya kwanza kwenda mlimani city, mara paa nakutana na mshikaji, ilikua kama sa 4 alafu hata sikua nimekunywa chai, tukakaa kwenye mgahawa, tukaagiza vitu vya kawaida kabisa. Bili kuja 60,000.00, na mfukoni nilikua na hiyo hivyo 60 ikabidi niende ATM pale niongezee kidogo ila nilichoka. Ilikua early 2010s.
 
Wewe unausingizi kalale kwanza ukiamka utaandika vizuri.
 
Popcorn za chumvi sio 4000 ni 3000.
 
Ukiona unalalamikia bei za vitu ujue baado una safari ndefu kiutaftaji mkuu.
Wewe kula kwa akina mama ntilie na uka jambie mbele ukipiga mluzi taratibu huku ukiendelea kukaza misuli kutafta kutafta pesa.

Usisahau kuwa pesa nayo inakumbukumbu na dharau.

itakukumbusha kila ukipita mlimani city kuwa hapa sio mahali pako wewe ni wa Tandale tu kwa akina Ashura😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…