Starlink wamekuja mara mbili kuomba kutuletea huduma ya internet lakini wanazungushwa, kuna ugali wa mtu unaguswa?

Starlink wamekuja mara mbili kuomba kutuletea huduma ya internet lakini wanazungushwa, kuna ugali wa mtu unaguswa?

Waafrika kupenda ushabiki , mnataka kila kitu amiliki Elon Musk ? Maana jamaa kila soko anavamia mpaka cryptos .

Wapeni kila kitu , watu wanalinda masoko ya ndani .Kampuni hizo za ndani zinatoa gawio kwa serikali na kusaidia kwenye mambo ya kijaa , sasa mleteni huyo mzungu ...Mtaanza kwa kusema ''wenzetu wa nchi fulani wanapata huduma as if kama unajua sasa '' mambo ni yale yale...

Acha ushabiki sio lazima watafute nchi nyingine.
Nani alikuambia hizi zilizopo ni kampuni za ndani ukitoa TTCL..Hayo makampuni yote ni ya kigeni yanavuna manoti..hiyo starlink na yenyewe ije TU , mwenye huduma nzuri achukue soko
 
Ni huduma yenye uwezo wa kuponya ukosefu wa internet vijijini, maporini, milimani, ziwani, n.k. ukizingatia kwamba makampuni ya mitandao ya simu yameshindwa kufikisha huduma katika maeneo ya mbali.

Kwa mara ya kwanza walikuja Tanzania bila mafanikio, waziri wa kipindi hicho Nape Nnauye alitoa sababu hawakuwakatalia starlink kufanya kazi Nchini, walikwama wenyewe, wengi tulipigwa na butwa kwasababu starlink walivyoondoka na kwenda Kenya wakapewa vibali bila shida na serikali ya Kenya kushukuru ujio wao utaopanua upatikanaji wa internet na kuleta ushindani utaoboresha huduma kwa makampuni ya mitandao ya simu

View attachment 3226961

Round ya pili wakarudi tena, ombi lao la kuomba leseni lilichapishwa lakini hadi sasa kuna kimya cha usiku wa manane

View attachment 3226947
JAMBAZI ROSTAM AZIZI NDIYE ANAYE KWAMISHA HIYO STARLINK
 
Subiri uchaguzi upite .. tunataka mtandao ambao tunaweza kuudhibiti
 
Nani alikuambia hizi zilizopo ni kampuni za ndani ukitoa TTCL..Hayo makampuni yote ni ya kigeni yanavuna manoti..hiyo starlink na yenyewe ije TU , mwenye huduma nzuri achukue soko
Unajua starlink inavyoendeshwa? Unajua mchango wa haya makampuni ?

Nchi ngapi Zina starlink mpaka Sasa? Hyo starlink Haina kipya kama hujui basi.
 
Elon Musk sio mtu wa kumuamini sana, ufanyike uchambuzi wa kina kama huduma yake haitaingilia na siasa zake.
 
Back
Top Bottom