Stars kuwakabili Uganda kesho Zanzibar

Stars kuwakabili Uganda kesho Zanzibar

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kesho inatarajiwa kushuka dimbani kucheza na timu ya Taifa ya Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainaili za wachezaji wa ndani CHAN 2016.

Kikosi cha Taifa Stars kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa kuanzia majira a saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo wa awali ili kujiweka katika mzingira mazuri ya kusonga mbele, kabla ya mchezo wa marudaino utakaofanyika baada ya wiki mbili jijini Kampala.

Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema vijana wake wako katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo wa kesho, na kuwaomba watanzania kuwapa sapoti katika mchezo huo.

Endapo Stars itaitoa Uganda katika hatua ya awali, itafuzu katika hatua ya pili ambapo itacheza dhidi ya timu ya Taifa ya Sudan, na mshindi wa mchezo huo moja kwa moja atafuzu kwa fainali za CHAN 2016 nchini Rwanda.

Wakati huo huo, timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili leo mchana jijini Dar es salaam kisha kuelekea kisiwani Zanzibar tayari kwa mchezo huo wa kesho dhidi ya Taifa Stars.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Best Regards,
Baraka Kizuguto
 
Hii mechi ingepigwa Taifa ningehamasisha wapenda soka wenzangu tungezama Taifa na bakora tu, ole wao wafungwe hatoki mtu kuanzia Jamali Malinzi mpaka dawati zima la TFF wapuuzi sana hawa,
Wanatafuna kodi zetu halafu wanarukaruka tu mbuzi hawa
 
Last edited by a moderator:
Hii mechi ingepigwa Taifa ningehamasisha wapenda soka wenzangu tungezama Taifa na bakora tu, ole wao wafungwe hatoki mtu kuanzia @JamaliMalinzi mpaka dawati zima la TFF wapuuzi sana hawa,
Wanatafuna kodi zetu halafu wanarukaruka tu mbuzi hawa

Labda mechi hii wanaweza kupata mafanikio....ngoja tusubiri matokeo.
 
watafungwa tu hiyo kesho hakuna matokeo zaidi ya hayo
 
Labda mechi hii wanaweza kupata mafanikio....ngoja tusubiri matokeo.

Watu Walimwambia Malinzi Kuwa Amfukuze Kocha Akawadharau Na Kuweka Pamba Masikioni Sasa Kwa Taarifa Za Kichinichini Ni Kwamba Kuna Wachezaji Waandamizi Wa Hivi Vilabu Vyetu " Big " Wameshashikishwa Mlungula Na Maadui Wa Malinzi ( Ambao Mimi Nawaita Mashujaa Na Wakombozi Wa Soka Letu ) Kwamba Kesho Wacheze Chini Ya Viwango Na Wafungishe Tena Kwa Makusudi Ili Tufungwe Kisha Mart Nooij Aondokee Huko Huko Zanzibar Na Kesho Tukihurumiwa Sana Wa Waganda Ili Tusije Kutafunana Tunapigwa Nguzo Tano au Wiki.
 
Kila la kheri...ila wa znz watakubali matangazo ya bia uwanjani mwezi huu wa ramadhani? Je mechi saa ngapi? Itaoneshwa?
 
Full TIME

Tanzania (Taifa Stars) 0 - 5 Uganda ( The cranes)
 
Tafadhali stars usiwe mwendelezo wa kipigo cha tano mfululizo bila hata kupata bao moja. maana mechi zilizopita tumepigwa goli nyingi kwa 0.
 
Hii mechi ingepigwa Taifa ningehamasisha wapenda soka wenzangu tungezama Taifa na bakora tu, ole wao wafungwe hatoki mtu kuanzia Jamali Malinzi mpaka dawati zima la TFF wapuuzi sana hawa,
Wanatafuna kodi zetu halafu wanarukaruka tu mbuzi hawa

ndio maana wapeleke huko, walijua mapemaa wale bodaboda ulikuwa ni mwanzo tu makubwa zaidi yangekuwa taifa.
 
Last edited by a moderator:
malinzi nilishawaambia ni specialist of failure hana jipya yule chenga tupuu na libabu lake
 
What is the logic behind kupeleka mechi Zanzibar? Mnisaidie labda kule kuna washabiki wazalendo! wengi pengine kushinda bara? au wanatarajia kupata mapato mengi kule..kwani najua mifuko ya viongozi wa awamu hii TFF "ilivyotoboka" kila kiingiacho "wanaswamilira"...
 
What is the logic behind kupeleka mechi Zanzibar? Mnisaidie labda kule kuna washabiki wazalendo! wengi pengine kushinda bara? au wanatarajia kupata mapato mengi kule..kwani najua mifuko ya viongozi wa awamu hii TFF "ilivyotoboka" kila kiingiacho "wanaswamilira"...

Siasa hkn lingine...mbaya wamesahau kuwa taifa stars wanadhaminiwa na bia ya Kilimanjaro...na huu mwezi mtukufu..znz km unaivyoijua..ktk mambo ya iman
 
Sioni sababu kubwa ya kupeleka mechi Zanzbar. Labda anayejua atujuze.
 
Taifa Stars ikitaka kushinda kesho ipangew hivi:

(1) Mwadini Ally
(2) S Kapombe
(3) Mwinyi Haji
(4) H Isihaka
(5) Nadir H
(6) J Mkude
(7) S Mdelwa
(8) A Banda
(9) S. Msuva
(10) A Kiemba
(11) Kelvin F

Sub: H. Dilunga, A. Green & R Mandawa
 
Back
Top Bottom