STARS kuwavaa Madagascar leo

STARS kuwavaa Madagascar leo

Hii timu haieleweki ni sayari ya ngapi,yaani ni kama vijana wamekutana na kuingia uwanjani utadhani ni maveterani ...mtangazaji anasema 30mns no shot on goal from Tz side,Kocha kaharibu na Mara hii tunakuwa Wa 200 kwenye rank

Ahaahaaaahaaaaa....
Maveterani kutoka Tanzania
 
hili timu linakera kwa kweli
oscar joshua sijui wametumia vigezo gani kuitwa national team
 
Na hapo imekaa kambi Botswana..Tukuyu..na itaenda Ethiopia..kuikabili Misri..teh teh teh..
 
Mbona lilikuwa wazi timu imeenda kufanya shopping.
 
hiyo sio timu ni mabishoo tu wameenda kuuza sura....kila mmoja anataka aonekane, bora wangeenda twiga stars
 
huyu kocha hamnazo anamtoa ngassa aliekuwa anasumbua kidogo na kumuacha bocco na luizio wanaozurura tu uwanjani
 
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo inashuka dimbani kucheza mchezo wake wa pili dhidi ya timu ya Taifa kutoka Madagascar, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Royal Bafokeng majira ya saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Taifa Stars inahitaji kupata ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Madagascar ili kufufua matumaini ya kuweza kusonga mbele katika hatua inayofua ya Robo Fainali.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars akiongelea mchezo wa leo amesema, makosa yaliyojitokeza katika mchezo dhidi ya Swaziland yamefanyiwa kazi na anaamini vijana wake watafanya vizuri.

“Mchezo wa Swaziland tulipata nafasi nzuri za kufunga, lakini washambuliaji wangu hawakuwa makini kuzitumia nafasi hizo, tatizo la kupoteza nafasi nyingi limefanyiwa kazi na nina amini leo vijana watafanya vizuri” alisema Nooij.

Aidha Nooij amesema anataarajia mchezo kuwa mgumu kutokana na Madagascar kuhitaji ushindi wa pili mfululizo, baada ya kuifunga Lesotho katika mchezo wa awali, Nooij ameahidi kufanya vizuri katika mchezo huo.

Mchezo huo utakuwa moja kwa moja (Live) katika kituo cha Superspot SS4, na SS9.

Naye kiungo wa Taifa Stars, Said Juma Makapu anarejea nyumbani leo usiku kwa usafiri wa Shirika la ndege la Fastjet kwa ajili ya kufanyia vipimo zaidi na matibabu, anatarajiwa kuondoka uwanja wa O.R. Tambo saa 5 usiku kufika uwanja wa JK Nyerer saa 8 usiku.

UCHAGUZI MKUU COASTAL UNION JULAI 5

Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limetangaza Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga utafanyika tarehe 05, Julai 2015.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Melchesedek Lutema ametoa ratiba ya mchakato mzima wa uchaguzi huo, ambapo tarehe 21-22 Mei mwaka huu zitatangazwa nafasi zote zinazogombewa.

Kwa mujibu wa kalenda hiyo ya Uchaguzi, tarehe 23-30, Mei 2015 itakua ni kipindi cha uchukuaji fomu kwa wagombea wote na kuzirudisha, wakati Juni Mosi mpaka Juni 04, 2015 ni kipindi cha mchujo wa awali kwa wagombea.

Juni 05, 2015 Kamati ya Uchaguzi itatoa orodha ya awali ya wagombea, Juni 7-9, 2015 itakua ni kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea, na Juni 10-11 ni kupitia mapingamizi yote.

Julai 02 -04, 2015 ni muda wa kampeni kwa wagombea wote na uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 05, Julai 2015.

Ratiba kamili ya mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Coastal Union imeambatanishwa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF


mshajambiwa huko...
 
Haha hili likocha Sijui TFF wamelitoa Wapi.....kwanini hwakumuacha Kim angalau timu ilieleweka?
 
Tatizo ni kocha, hivi kwa nini tusimuazime babu wa Yanga? maana tuwe wakweli, ameikuta Yanga inacheza hovyo, akafanya kazi nzito, na kweli tumeona mabadiliko makubwa katika kupanga mashambuli, na kujilinda.
 
Back
Top Bottom