Kilakshari
JF-Expert Member
- Dec 13, 2008
- 350
- 20
Mechi inachezwa saa ngapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mechi inachezwa saa ngapi?
[/TD]
Mechi inaanza saa nne na nusu usiku kwa saa za Afrika mashariki (22hr30). Tujipe moyo tu na kuonyesha uzalendo lakini ukweli ni kwamba hatuendi popote tunakamilisha ratiba tu!
Nimesikia TBCccm mkuu!Kuna kituo kitarusha live mechi hii?Nina hamu kuangalia mechi hii kupima maendeleo yetu.Kiufundi Poulsen yupo safi sana kwani angalau sasa Taifa stars wanamiliki mpira.
Yeah, kule Morocco, saa hizi ni saa nane, na wao ni GMT + 0, Tanzania ni GMT + 3ni saa tano kasoro robo usiku..
Kuna kituo kitarusha live mechi hii?Nina hamu kuangalia mechi hii kupima maendeleo yetu.Kiufundi Poulsen yupo safi sana kwani angalau sasa Taifa stars wanamiliki mpira.
kwa jinsi unavyowaabudu waarabu nilidhani ungeweka uzalendo pembeni na kutaka waarabu washinde! big up lady!
Unaujua mpira au unazijua fitna za bongo?Huwezi kumfananisha Poulsen na Julio(nasikia ndio anafanya form four!).Wabongo tunaongoza kudharaua elimu.Julio amefanya nini au umeisikia timu ipi ameifundisha angalau tu ikacheza mpira?Maneno yake ya 'kibongobongo' yanawachanganga wengi.Kocha unaulizwa unaionaje Nigeria,unajibu Nigeria ni sawa na uji!Again,akaulizwa unauchukuliaje mchezo na Uganda,akajibu 'Uganda walibebwa na refa.Matokeo tuliyaona wenyewe.Tuache uswahili,oh Mzungu...mweupe!Makocha wakibongo waende shule kwanza kabla ya kupewa timu ya taifa.Tulishindwa kuwafunga wale Central African Republic itakuwa Morroco Bao hizo 4 labda kushinda bao 2-1 tukubali yaishe basi. Tuombe Taifa Stars wafanye ya Niger walivyompiga Egypt kwao 3-0. Kuhusu Mwalimu mie naona tumuweke Fundi wa Vijana mzungu atolewe na fundi wa Vijana alipwe kama anavyolipwa Mzungu yule hana upendeleo wa wachezaji wapo wazuri wengi timu za mikoani na visiwani si Yanga na Simba tu na timu za Dar-es-salaam zimejaliwa kuweka wachezaji timu ya taifa.
Nawatakia kila la kheri vijana wetu wanaotupeperushia bendera yetu huko. Nawaombea wawe mabalozi wema na warudi na ushindi.
Ila wakishinda tu utaona siasa zinaanza. Na yale magazeti (Uhuru, Habari leo etc.) watabadili na kuwaita JK Eleven (badala ya Taifa Stars), etc. Kila la heri Stars!
Mbona Ngassa sikuhizi anaanzia bench? Kiwango kimeshuka au nini?4-4-1-1 Ndio atatumia leo Fundi Poulsen Taifa Stars: Juma Kaseja,Erasto Nyoni,Idrisa Rajab,Juma Nyoso,Agrrey Morris,Shaaban Nditi,Mohamed Rajab,Henry Joseph(C),Mbwana Samata,Abdi Kassim,Dan Mrwanda.
Bench😀ihile,Nassor cholo,John Bocco,Ramadhan Chombo,Mrisho Ngassa,Nadir Haroub,Jabir Aziz. Nimeipata Blog Flani.