Stars wasingizia baridi kipigo cha Ethiopia

Stars wasingizia baridi kipigo cha Ethiopia

Gmark

Senior Member
Joined
Nov 6, 2015
Posts
138
Reaction score
30
Hivi taifa stars waache kujitetea, waseme tu wanapaswa kuwekeza zaidi.

Kule kwa waarabu waliona wamefanyiwa tricks nyingi, mara Mpira unadunda sasa hii ya kuchapwa na Ethiopia, baridi iliwachosha. Kwa nini hawakujifulia Arusha au Iringa?

Pia wamefungwa kwa penalties sasa hiyo baridi inaingiaje? Wajifue na wajitoe zaidi tu banaa
 
Hiyo team haibebeki hata ifanywaje!
 
Ningekuwa mimi ni Magufuli ningesimamisha ushiriki wa hii timu kwenye michezo ya kimataifa kwa miaka 5 ijipange upya
 
Ningekuwa mimi ni Magufuli ningesimamisha ushiriki wa hii timu kwenye michezo ya kimataifa kwa miaka 5 ijipange upya

Kisha ili kuondoa umasikini watanzania wote wasifanye kazi kwa miaka 5 ili wajipange upya. What do you think?
 
"Waarabu walitushinda kwa taaaaabu sana..,wahabeshi ilikuwa bado kidooogo tuwafumue...!hata hivyo tumeondolewa kishujaa."tusubiri kusikia Kauli Kama hizi za kujipoza..halafu basi!!!
 
Kuna mtu yeyote anaetaka kuja taNzanIA tubadilishane jamani nauliza!! kuna mtu yoyote anataka kubadilishana uraia na tanzania? hakuna jibu!
 
Kuna mtu yeyote anaetaka kuja taNzanIA tubadilishane jamani nauliza!! kuna mtu yoyote anataka kubadilishana uraia na tanzania? hakuna jibu!
Nipo hapa mkuu Ila mie nipo Syria huku kwa ISIS vp twaweza badilishana
 
Ningekuwa mimi ni Magufuli ningesimamisha ushiriki wa hii timu kwenye michezo ya kimataifa kwa miaka 5 ijipange upya

Unajua sheria za FIFA kuhusu serikali kuingilia issue zauongozi wa mpira ?
 
Hivi taifa stars waache kujitetea, waseme tu wanapaswa kuwekeza zaidi.

Kule kwa waarabu waliona wamefanyiwa tricks nyingi, mara Mpira unadunda sasa hii ya kuchapwa na Ethiopia, baridi iliwachosha. Kwa nini hawakujifulia Arusha au Iringa?

Pia wamefungwa kwa penalties sasa hiyo baridi inaingiaje? Wajifue na wajitoe zaidi tu banaa

Kwahiyo Hata Zile Penalties Mbili Za Watoto Wa Morogoro Mkude Na Kapombe Baridi Hilo Kali Liliingia Miguuni Mwao Hadi Kubadilisha Muelekeo Wa Upigaji Penalties Zile Za KIPOPOMA Kabisa Na Kumpa Goalie Wa Ethiopia? Wengi Tumeangalia Huo Mpira Ila Sasa Nataka Kuungana Kabisa Na Zile MAKALA KUU SABA ( 7 ) Za Comrade Wangu Saleh Ally a.k.a JEMBE Kuhusiana Na MAPUNGUFU MAKUBWA Ya Soka La Bongo. Ziko MAKALA SABA TU Na Kama Mnaweza Zitafuteni Kupitia MTANDAO Wake Wa SALEHJEMBE Mjue Mengi. Nimesoma Na Nimejifunza Mambo Makubwa Na Hakika Huyu Jamaa Mwandishi Saleh Ally Wa Gazeti La Champion Hana MPINZANI Hapa Tanzania Hasa Ktk MASUALA Ya UCHAMBUZI Na UANDISHI Wa MICHEZO. Ktk Hizo MAKALA Zake Kuu 7 KUNA MAMBO MAZITO ALIYOYAFICHUA Na Hasa Hasa Kipindi Cha MAANDALIZI Ya Mechi Ya Algeria, Kambi, Nidhamu Ya Wachezaji Wetu, Maandalizi, Uadilifu Wa Viongozi Wa TFF Na Hadi Kamati Ile Ya Saidia Stars Ishinde Na Hadi Ameelezea Jinsi Gani Mtu Anayejifanya Ni MCHAMBUZI Wa SOKA LA TANZANIA Shafii Dauda Alivyokuwa MNAFIKI Na MSALITI Kwa Taifa Lake. Hakikisheni Mnazisoma Na Kuzielewa Hizo MAKALA SABA Ktk Huo MTANDAO Wake.
 
Mi nadhani tuanze upya tu kutengeneza timu ya taifa hizi short cuts hazitatusaidia
 
Baridi?!
Kwani wenzao walicheza huku wamevaa Makoti ya kujikinga na baridi?!
 
Kibaden na genge lake wawekwe lock up. Timu ya Ethiopia ni mbovu sana ktk mashindano haya na haiwezi kufika popote japo ni wenyeji.

Kwa watu serious Kilimanjaro ilipaswa kutwaa ubingwa huu au angalau kucheza fainali.
 
Back
Top Bottom