Stars yapoteza Mchezo wa Pili

Stars yapoteza Mchezo wa Pili

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) jana imepoteza mchezo wa pili mfululizo katika michuano ya kombe la Cosafa, baada ya kufungwa mabao 2 - 0 na Madagascar, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg.

Kwa Taifa Stars kupoteza mchezo huo, moja kwa moja inakua imeaga michuano katika hatua ya makundi, kutokana na kubakisha mchezo mmoja tu wa kukamilisha ratiba dhidi ya Lesotho utakaochezwa kesho ijumaa katika uwanja wa Moruleng.

Katika mchezo huo wa jana, Taifa Stars ilishindwa kuonyesha makali yake mbele ya timu ya Madagascar na kupelekea kufungwa mabao 2 katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Sehemu ya ushambuliaji ya Taifa Stars haikua na madhara yoyote langoni mwa Madagascar, huku sehemu ya ulinzi iLijikuta na wakati mgumu muda wote kuzuia hatara za washambuliaji wa Madagascar.

Mara baada ya mchezo huo, kocha wa Stars Mart Noij alisema amesikitishwa na matokeo hayo, kwamba hakutegemea kupoteza mchezo dhidi ya Madagascar.


"Timu yangu haikucheza vizuri, haikuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga , huku wapinzani awetu wakitumia nafasi mbili walizozipata kupata mabao mawili katia mchezo huo" alisema Nooij.


Mpaka sasa kundi B la linaongozwa na Madagscar yenye ponti 6 sawa na Swaziland yenye pointi 6 pia zikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, na mchezo wa mwisho utakaowakutanisha kesho ndio utakaoamua nani atatinga hatua ya robo fainali.

Kufuatia Taifa Stars kupoteza michezo yote miwili, inaungana na Lesotho kutoka kundi B kuaga michuano hiyo, huku kundi A timu za Mauritius na Shelisheli zikiwa zimeshaaga michuano hiyo pia.

Stars inatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania kesho iumaa usiku mara baada ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho utakochezwa kesho jioni.

KAMATI YA UTENDAJI YA TFF KUKUTANA MEI 24

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF inatarajiwa kukutana jumapili tarehe 24, Mei mwaka huu ikiwa ni kikao cha kawaida cha kamati hiyo.

Moja ya ajenda katika kikao hicho itakua ni kupokea na kujadili mienendo, maandalizi na maendeleo ya timu zaetu za Taifa za mpira wa miguu nchini.

NB: Picha za mchezo wa jana kati ya Tanzania dhidi ya Madagascar
zimeambatanishwa

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
 
Na mpira umekwisha, tumepigwa kimoja na LESOTHO! Aisee!! Sijui ndio tumetolewa kishujaa au ndio nini??? Kocha hatakosa sababu!!! Tunafungwa hata na LESOTHO???????
 
Hivi tulilazimishwa kwenda kwenye hayo mashindano? Ni bora tungebaki home kuliko kwenda kutia aibu namna ile....hakuna cha kujifunza wala nini kwani hawakuwa na uelewano wowote uwanjani.....sijui tulikuwa tunacheza soccer au kiduko!!!
 
Hao ni watalii tu na wamekutana na mibunye ya Kisouth imewalegeza kuanzia kocha mpaka wachezaji.....watanzania tutashinda michuano ya kugombania mibunye tu......
 
Hivi hawa si kuna timu yao ilishapigwaga na pamba ya mwanza goli 14? Ilikuwa inaitwa Anserbaloon, kitu kama hicho!

Japo haikuwa timu ya taifa, ila ni kweli ilikuwa timu kutoka huko Madagascar,ilisambaratishwa kwa goli hizo 14.

Hata sasa, bado Madagascar wabovu ki mpira, inashangaza sana Taifa Stars kuboronga kwa hao jamaa.

Swali linajirudia, kweli hata Madagascar wanatufunga 2-0????
 
Back
Top Bottom