Stars yapoteza Mchezo wa Pili

Stars yapoteza Mchezo wa Pili

timu yetu imefungwa michezo yote iliyocheza
 
Tukisema Yanga inanunua mechi mnapiga kelele... Aya Yanga aibu yenu hiyo maana nyie ndio mmejaa huko Taifa Stars
 
Tatizo kocha, unakumbuka alikua Maximo mwaka jana tulimfukuza na akaja huyu wa sasa, wachezaji walewale mwarabu jasho ilimtoka. Tumeuza wachezaji kule sasa wametia aibu.
 
Japo haikuwa timu ya taifa, ila ni kweli ilikuwa timu kutoka huko Madagascar,ilisambaratishwa kwa goli hizo 14.

Hata sasa, bado Madagascar wabovu ki mpira, inashangaza sana Taifa Stars kuboronga kwa hao jamaa.

Swali linajirudia, kweli hata Madagascar wanatufunga 2-0????
Siyo kweli mkuu, pamba iliwafunga washelisheli goli 12 na baadae ikakutana na BTM ya madagascar kabla ya kuondoshwa mashindanoni na villa ya uganda.
 
Siyo kweli mkuu, pamba iliwafunga washelisheli goli 12 na baadae ikakutana na BTM ya madagascar kabla ya kuondoshwa mashindanoni na villa ya uganda.

Mkuu, asante kwa kuweka rekodi sawasawa.

Hoja yangu, bado iko palepale, iwe Shelisheli au Madagascar sioni uwezo wao wowote kisoka kutizidi Watanzania.

Hii ni aibu, bado tujiulize tu: hata Madagascar....???
 
Wakati wanapoteza mechi ya kwanza na kutokana na kiwango walichoonyesha nilisema tutatoka kwa aibu tena kubwa. tunafungwa na vinchi vidogo ambazo zote zikiunganishwa haifikii hata mkoa 1 kwa ukubwa. Nashauri kila mkoa au wilaya ianze mpango mkakati wa kuanzisha mashindano ya kuboresha timu ya taifa. waache tabia ya kuokota wachezaji DSM walioharibiwa na chips mayai. Kiukweli nimeumia roho.
 
huyo Nooij ni agent wa wakoloni nin?..katumwa kutuhalbia cv zetu....asikanyage tena Tanzania apitile kwao Uholanzi ala!
 
Tukisema Yanga inanunua mechi mnapiga kelele... Aya Yanga aibu yenu hiyo maana nyie ndio mmejaa huko Taifa Stars
Ndemla, mbonde, luizio, kazimoto, kapombe, bocco, hajibu, nyoni, Mngwali hao wote wanachezea yanga!?
Jamii forum imeingiliwa hata wewe nawe?!
 
Nilisema Tangu mwanzo...Ulikuwa ni Upuuzi wa hali ya Juu malinzi kumfukuza Paulsein....Haya ndiyo matokeo sasa Jamal Malinzi
 
Last edited by a moderator:
Tukisema Yanga inanunua mechi mnapiga kelele... Aya Yanga aibu yenu hiyo maana nyie ndio mmejaa huko Taifa Stars

Yanga wapo wangapi kwenye timu? Tatizo kuchanganya na mchangani ndio maana ipo Hovyo!
 
Hata mkimteremsha Mungu kwa hiyo timu tutafungwa tu. Tumeshabadili makocha sana. Sasa tuwafukuze hao wachezaji wote tuanze upya,hawafundishiki tena,uwezo wao umefikia kikomo. Kenya walijaribu wakaweza,wakapata timu nzuri ya ushindi na mabadiliko yalionekana ingawaje kwa sasa nao wameanza kuchoka. Tuvunje Taifa Stars,wachezaji ndio tatizo sio makocha
 
Tukisema Yanga inanunua mechi mnapiga kelele... Aya Yanga aibu yenu hiyo maana nyie ndio mmejaa huko Taifa Stars

Kuna baadhi ya members sijui wametokea Mirembe! Wanaona kwenye hiyo list kuanzia namba 1 mpaka 20 wote karibia ni wachezaji wa Yanga
 
Attachments

  • 1432362550210.jpg
    1432362550210.jpg
    74.3 KB · Views: 87
huyo Nooij ni agent wa wakoloni nin?..katumwa kutuhalbia cv zetu....asikanyage tena Tanzania apitile kwao Uholanzi ala!

Wangekua wenzetu wa West Africa, huyu kocha angepanda ndege ya kuelekea kwao akitokea huko huko South lakini sisi tutamuacha aje hapa na siasa zitachukua nafasi yake, mholanzi utamuona akiendelea "kukinoa" kikosi cha Stars. Afadhari tusiwe na kocha wa nje.
 
Kikosi chote cha Taifa Stars kifumuliwe kisukwe upya.
 
Back
Top Bottom