Startimes kuja na huduma za DTH

StarTimes Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
260
Reaction score
141
Ili kuwezesha huduma zetu kupatikana, maeneo yote ya Dar es Salaam, startimes inategemea kuzindua huduma ya satellite dish ambayo itatoa fursa kwa wakazi wote wa Tanzania kupata huduma za startimes. Chanel katika receiver za satellite receiver zitakuwa ni nyingi zaidi ya hizi zilizo katika mfumo wa DTT

Pia Startimes tumefanikiwa kuinunua kampuni ya TOP TV ya africa kusini na hivyo kufanya huduma za startimes kuanza kupatikana pia SOUTH AFRICA. Kwa mantiki hiyo huduma za startimes kwa sasa zinapatikana katika nchi zisizopungua 15 Africa na tunategemea kufungua huduma zetu katika nchi nyingine

Pia tumefanikiwa kuanzisha huduma ya MOBILE tv Kwa mkoa wa Dar es Salaam pia Arusha na tunategemea huduma hii kuenea tanzania mzima.
 
bado tuelekeze mnara kisarawe?
 
 
Arusha ving'amuzi tu vimewashinda kurekebisha, vikataka kata sana baadhi ya maeneo, hyo ya simu ndo mtaiweza? Kuwepo nchi 15 kunanisaidia nn mm mtanzania kama hapa Tz tu huduma inasuasua?. "Small is beautful", kma bado hamjajiweza ni bora mkawa eneo dogo na mkatoa huduma kwa ufasaha
 
Startimes,sisi wateja wenu tunataka mboreshe station,sisi kama wateja wenu tunakosa huduma nyingi za soka mna shindwa nini kutuwekea station 1 au 2 zitakazokua zinatuonyesha mipira? Kama mna weza kununua kampuni ya africa ya kusini nini kinawashinda kusikia kilio chetu cha muda mrefu? Niaibu kuwa na kingamuzi chenu tena mnajitapa ninyi ni kampuni kubwa mnashindwa kutuwekea ligi ya uingereza? Embu jitafakarini kwa kina kama mnataka kuteka soko la tanzania,
 
ili nipate super sport zote natakiwa kulipia kifurushi cha bei gani? na je ving'amuzi vyenu vya sasa vina uwezo wa kurekodi?
 
 
sijawai kuona huduma mbovu kama ya hawa jamaa ...dar tu imewashinda.....azam ndo kiboko yao wewe ngoja tu...wataangalia telenovela zao wenyewe
 
Tatizo c kupatikana nchi kumi na tano za afrika ! Je huduma mnazowapa wateja wanaridhika nazo?hapa dar tu matatizo unaweza kukaa cku tatu huoni chanel yoyote na mtu umelipia kisa signal weak mala no service! Hata kama mkipatikana dunia nzima kama huduma zenu ndio hizi hizi haitakuwa na maana, na ndipo mtapata hasara kabisa kwani huko watoa huduma wapo wengi na huduma bora si hapa tz ushindani hamna wote ni wale wale tu.
 
 

Nina maswali hapa chini yanahitaji majibu,

1.Wakati mnasajili kampuni pale Brela,mliandika kuwa mtafanya kazi Tanania bara pekee na Zanzibar haiwahusu?

2.Je na Zanzibar mlisajili kampuni nyingine ya Star times?

3.Kama sivyo,kwanini ving'amuzi nyenu mnavyouza bara haviwezi kufanya kazi Zanzibar vivo hivyo kwa vinavyouzwa Zanzibar?

4.Je kama leseni yenu ya biashara mlichukua kwa ajili ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwanini ukitoka na king'amuzi bara ukifika Zanzibar unaambiwa ulipie shilingi elfu sitini(60,000) ndio uweze kupata huduma Zanzibar?

5.Je ukinunua king'amuzi dar ukienda nacho Arusha hakifanyi kazi mpaka ulipie elfu sitini(60,000) ndio niweze kuona wakati ni ndani ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania?

Nahitaji majibu ya maswali hayo na ukishindwa kujibu na kuleta visingizio ujue nyie ni wezi na wababaishaji na ni kati ya makampuni mengi tu yanayofanya wizi mkubwa kwa watanzania.


 

wise boy, habari yako, wateja wetu wengi arusha wanafurahia huduma zetu, kugandaganda kwa picha kunatokana na ufungaji usio sahihi wa antena yako au matatizo ya king'amuzi chako, tafadhari jaribu kuwasiliana na kituo cha huduma kwa wateja arusha watakupatia msaada ufurahie huduma zetu
 
 

swali: Epl mnatuwekea lini? Na kwa nini hamtaki kutupa burudani ya soka? Na ninyi ni kampuni kubwa??
 

Mkuu hebu fafanua zaidi hapo kwenye blue text....
Dish yenu itakuwa na channel ngapi, unaweza kuzitaja..??
 

White wizard, no signal au no service inamaana hupati mawimbi yetu ipasavyo, tafadhari fuata maelekezo unayopatiwa toka vituo vyetu vya huduma kwa wateja au kitengo cha huduma kwa wateja 0764700800 ili nawe ufurahie huduma zetu nzuri zaidi

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…