StarTimes Tanzania
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 260
- 141
Kwa muda wa zaidi ya wiki mbili kuna maeneo kadhaa hapa nchini pamoja na nyumbani kwangu, ambapo matangazo ya ITV & EATV (Startimes) yamekuwa yanakwama sana na kutoa picha mbaya na tena ni kuanzia saa 11 jioni hadi saa 5 usiku. Sasa ni hivi kwa upande wangu ninapoona matangazo ya ITV hayaonekani vizuri huwa ni bora nikazima TV kuliko kuangalia habari ya TBC.
Nawasilisha wakuu.
KILAKA.
Karibu sana JF StarTimes Tanzania
Mjibu mdau hapa.
Au bofya hapa
https://www.jamiiforums.com/habari-...2-itv-and-eatv-wanahujumiwa-na-startimes.html
kitokana na kutoonekana vizuri kwa ITV katika kingamuzi cha STAR TIMES wakati wa taarifa ya habari katika maeneo mbalimbali nchini hususani mkoa wa DSM inasekana kuna taarifa za kukihujumu kituo hicho kikongwe nchini.Baadhi ya vingamuzi kama vile CONTINENTAL,DSTV,AZAM TV,EASY TV,wakati wa taarifa ya habari ITV inaonekana vizuri sana lakini kwa star times inakatika katika hovyo hadi watazamaji wa ITV wanashindwa kutazama taarifa za habari vizuri.mwandishi alipokwenda katika ofisi za sta times walimpoga chenga kwamba hawako tayari kuzungumzia hilo jambo,kama vile haitoshi mwandishi akamlazim kwenda katika mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA prof. Mkoma alijibu ana wageni anawasubili.Hivyo katika kingamzi cha star times ITV inahujumiwa.
Mie nimesahau nambari yangu ya siri, hivyo nikiingia pale setting nashindwa kupata access, msaada wenyu tafadhali
Kuna jirani yangu hivi karibuni king"amuzi chake startimes kimeibwa achukue hatua gani licha ya kuwa amesharipoti polisi ?
mkuu pole sana mimi nilikuwa na tatizo hadi nikahama nilifikiri ni eneo nililipo.Ila nawashukuru sana ITV kwa kuwa wameweza kunisemea tatizo langu nitaangalia leo kujua kama limeisha.Habari yako
Tafadhali ingiza namba siri '0000' kisha ukiingia katika 'SETTING' nenda katika 'PARENTAL CONTROL' option na chagua 'OFF' kama ukiingiza hiyo PIN itakataa tafadhari tunaomba ufike katika ofisi zetu kwa msaada zaidi
Swali : Naomba kufaham bei ya king"amuzi chenu ni kiasi gani kwa sasa mana huku mtaani kila mtu anataja bei yake ?
Hellow startimes! king'amuz changu kinasumbua sana channel nyingi zina scratch especialy muda wa jioni nashindwa kuangalia TV kabisa tafadhali naomba msaada wenu npo maeneo ya mbagala na number ya smart card 02035351569
Karibuni sana Star media JF, Mjiandae kupongezwa pia kukosolewa na wanaokosoa wanawapenda kiasi cha kuwaambia udhaifu(holes) kwenye huduma zenu ili kesho muwe washindani bora kwenye soko lililojaa ushindani.
Karibuni uwanja huru.