Habari za mdaa huu wanajamvi wenzangu,
Nimeamua kuandika uzi huu kwa wanaJF wenzangu ili kuwajuza kuwa kampuni kubwa na ya kwanza kuingia nchini kwetu ya Ving'amuzi aina ya STARTIMES ni wababaishaji,pia huduma zao zimembana mteja kwa maana nyingne vifurushi vyao ni ghali sana.
Jana STARTIMES huduma kwa wateja walinipigia simu mida ya saa nne na robo,nikaamua kupokea na kusikia sauti ya nzuri na ya ukarimu kutoka kwa muhudumu wao wakike,kisha akaniambia tunapenda kukutaarifu kwamba tuna offer kwa wateja wetu inayoendelea sasa katika ving'amuzi vyetu.Ukinunua kifurushi cha kuanzia buku sita unapata offer ya kuangalia chanels za packages nyingine kama vile smart pack ana uhuru,nikawajibu sawa lakini ni siku tatu tu zimepita tangu nilipie kifurushi cha mambo na sijaona chochote,akanijibu kwamba niliwahi kujiunga kabla ya offer yao ambayo ilianza 1st April,nikamuuliza je nikijiunga na sasa hv ntapata kuona hzo chanels zote?Akaniambia definetly nitaziona.Basi mimi nikaamua kulipia tena na kusubiri about 45mins. bila mafanikio yoyote,nikaamua kuwapigia simu kwakutumia ile namba yao ya customer service na ikapokelea nikapewa maelezo ambayo mimi naweza kuyaita poorer,wrong and fake instractions kutokana hayukuweza kufanya kazi hata mpaka sasa kwani nilibaki kuambiwa just wait for 15 mins then utazikuta,mara mwingine weka TBC1 for 15 mins then utakuta tumekuwekea mara ya mwisho kabisa nikaulizwa ni mtoa hudumayupi aliyekupigia simu.Nikamwambia akawaulize voda au TCRA kwani ndo wenye mamlaka na wateja wao.
Tatizo lingne la hawa majamaa ni kwamba voucher yako ikikata wanakubakizia chaneli mbili tu ambazo ni TBC1 na TV1.
PENDEKEZO;Kwa wateja wapya wenye mpango na hilo likampuni la startimes ni vyema kuchagua ving'amuzi vingine kwani startimes hawana huruma wa hawajali wateja wao.
PLEASE,DON'T BE FOOLED BY THE MASKS THEY WEAR,MAKE YOUR RIGHT CHOICE USIJE UKAJUTIA PESA YAKO.