Statute of Limitations

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Nimesoma kuwa mtu mmoja kafungua kesi huko SA akitaka ndege ya ATCL ikamatwe kwa sababu anaidait Tanzania mali zake zilizotaifishwa na Nyerere mwaka 1967. Je Statute of Limitations haifanyi kazi kwenye mazingira haya. Ataletaje kesi ya miaka 52 leo- hata miaka 10 tu, kwani hata ushahidi hauwezi kuwa verified tena?

Haya wanasheria , toeni ufafanuzi, hii imekaaje?

UPDATES: Ni mali zilizotaifishwasmwaka 1982, siyo 1967.
 
Nenda ofsini kwa Wakili akupe ushauri/ ufafanuzi. Hii ni noble profession. Hivyo ushauri/ ufafanuzi wa mwanasheria au Wakili lazima uulipie. NO FREE LUNCH.
 
Nenda ofsini kwa Wakili akupe ushauri/ ufafanuzi. Hii ni noble profession. Hivyo ushauri/ ufafanuzi wa mwanasheria au Wakili lazima uulipie. NO FREE LUNCH.

Tambalism at its best face.

Niliweka hapa kwa ajili ya watu kujadiliana tu, siyo kwamba siijui mzee. Kwanza hata kuianzisha mada yenyewe ni kwamba ninaijua. JF ni sehemu ya watu kuelemishana na kubadilishana mawazo, post yangu tu ilikuwa ni elimu kwa wengine, na netegemea watu wengine pia wataongeza kidogokidogo kadri mada inavyokwenda. Wewe hukuongeza kitu kwenye somo na siyo lazima kila msomaji aongeze kitu; inawezekana hulijui.

Sasa kama ulikuwa hujui, nimekuwekea kopi iliyotolewa na wanasheria wengine hapa; inaweza kukusaida kujua jambo lenyewe.
 

Attachments

The Law on limitation is not absolute. In appropriate cases and situation it can be extended as courts deem fit and appropriate.
 
Nimejiuliza sana... haya madeni ni ya zamani sana...

Why now?


Cc: mahondaw
Haya madeni yamefufuliwa na watanzania wenyewe ambao ama wamekoseshwa business as usual iliyokuwa inawaingizia utajiri mkubwa sana au wanaotaka serikali ya sasa ishindwe kazi kusudi wapate uraisi mwaka kesho. Kwa mfano serikali ya sasa ingekuwa business as usual usingesikia kesi hii; ni ya zamani sana mpaka imeshapitwa na muda kisheria. Iwapo serikali itakuwa na jopo zuri la wanasheria kuhusu kesi hiyo ya Afrika ya kusini, huyo mkulima atalimwa sana. Kuna mapungufu makubwa katika kesi yake hiyo baada ya makubaliano yale aliyoingia mwaka 1991 hata kama hakulipwa. Kuna taratibu hakuzifuata katika kuomba ndege hiyo ikamatwe, ndiyo maana kwenye list ya washitakiwa wake ameunganisha makampuni kadhaa ya Afrika ya Kusuini ambayo hayahusiki kabisa na mgogor baina yake na serikali ya Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…