Stbongo Tv Nyerere Day 2022

Stbongo Tv Nyerere Day 2022

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
BONGO TV NA NYERERE DAY

Kevin Lameck wa Bongo TV leo asubuhi alinitembelea nyumbani kwa nia ya kufanya kipindi cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya Nyerere Day kesho.

Bwana Kevin kanirushia maswali mazito moja akitaka kujua kama historia ya Mwalimu imekamilka anaenziwa kama inavyostahili.

Tulipita kwa pamoja vitabu vya waandishi ndani na nje waliomuandika Mwalimu na historia ya uhuru wa Tanganyika mfano wa John Hatch, Judith Listowel na mimi mwenyewe.

Kevin aliporomosha maswali mengi mengine ya kuogofya akichambua historia ya Baba wa Taifa na kutaka kupata yale ya mchagoni ya Baba wa Taifa kutoka kwangu.

Kevin ni kijana mjanja.

Nikilikwepa swali kwa kummwagia mengine hakuwa anakawia kunirejesha kwenye mstari huku akitabasamu.

Kuna kipande akitaka kujua msimamo wa Mwalimu katika mkondo Tanganyika itachukua itakapokuwa huru.

Kwa ujanja alikuwa ananiuliza Ujamaa wa Mwalimu sera iliyokuja kuathiri mstakabali wa uchumi wa Tanzania ilitokea wapi?

Nilimkwepa yeye na swali lake nikitaka alitafute jibu mwenyewe kwenye mazungumzo yetu.

Nikamvurumishia wazalendo "siasa kali," ndani ya TAA na ndani ya Kamati ya Siasa ya (TAA Political Subcommittee) mfano wa Hamza Mwapachu na Steven Mhando na uhusiano wao na Fabian Society.

Hawa walimtangulia Mwalimu Nyerere pale TAA New Street kwa kitambo kirefu.

Kutia nguvu hoja yangu nikamtolea kitabu cha John Hatch mmoja wa wanachama wa Fabian Society aliyekuwa karibu sana na TANU.

Naamini kipindi hiki kitaongeza elimu katika historia ya Mwalimu Nyerere.

1665696483449.png
1665696518179.png
1665696581386.png
1665696612573.png
 
Back
Top Bottom