STEALTH (LOW OBSERVABLE) TECHNOLOGY | Teknolojia ya ndege kutoonekana/kutotambulika na rada (RADAR)

Kwa iyo ile waliyotungua serbia kwa kutumia s-125 Neva/pachora sio yenyewe ?
NI yenyewe lakini nilivyomwelewa Mimi mwandishi ni hivi so kwamba haiwezi kabisa kuonekana but Ina kiwango Cha chini kabisa Cha signal kuweza kuonekana kirahisi.
Kwa hiyo f 117 iliingia kwenye mikono hatari zote zilionekana zikashushwa kwa pupa
 
NI yenyewe lakini nilivyomwelewa Mimi mwandishi ni hivi so kwamba haiwezi kabisa kuonekana but Ina kiwango Cha chini kabisa Cha signal kuweza kuonekana kirahisi.
Kwa hiyo f 117 iliingia kwenye mikono hatari zote zilionekana zikashushwa kwa pupa
Teknolojia hii ya STEALTH inafahamika kama LOW OBSERVABLE TECHNOLOGY. Kama nilivyosema hapo awali, kupitia mbinu mbalimbali, teknolojia hii inakipatia chombo uwezo wa kutotambulika ama kutoonekana kirahisi na mifumo ya utambuzi. Ndio maana ya maneno "Low Observable".
 
Franc The Great umeelezea vizuri sana kuhusiana na STEALTHY TECH. kiukweli technology hii ipo katika nchi nyingi lakini wanao ongoza ni USA and Russia, lakini nataka nikwambie kwamba utimilifu au umadhubuti wa technoloji husika itategemea umeenda kuitumia kwa nani.

Yapo mataifa duniani hutasikia wakieleza ufundi na ujuzi wao ila ukijichanganya ndo utaelewa kwamba unahitaji kuanza upya kabisa au hiyo tech. imeshakuwa outdated.

mara nyingi US wamekuwa wakiongeza chumvi na propaganda juu ya uwezo wao wa technology. Samahani nitatoka nje ya mada ili kuweka kumbukumbu sawa.

Wengi mtakubaliana nami kuwa ni ukweli usiopingika kwamba US ana tech. nzuri ktk medani za vita lakini pamoja na umahiri wake huo kuna wakati huwa anaongeza chumvi na ku exergarate uwezo wao kuliko uhalisia ipo mifano mingi, mojawapo ni ule wakati wa Clandestine Aerial Espionage 1960s, wakitumia Peshwar Military Air base huko Pakistan

Walitumia ndege za kipelelezi za Lockheed Martin aina ya U 2 Spy plane ambazo waliitangazia duania kuwa ni high tech inapita juu sana haitunguliwi lakini ilitokea aibu baada ya Francis Garry Powers kudunguliwa na kupatikana akiwa hai.
Pili kule Serbia ambako lilidunguliwa dege linaitwa F-117 A liliokuwa na sifa kedekede eg Stealth etc.

Nimalizie tu kwamba hizo tech zipo ila kuna mahala ukiingia nayo wanakufumua asubuhi tu hivyo tunaheshimu uwepo wa technology but u need to be extra careful hasa ukiingia vitani na Giants.
 
Ongezea na ile drone isiyoonekana kwenye rada mashia wa iran wakaitungua.
 
Nakushukuru kwa mchango wako.

Teknolojia hii ina changamoto mbalimbali. Moja ya changamoto hizo ni katika uwepo wa hizi countermeasures dhidi yake. Teknolojia hii inapozidi kuboreshwa zaidi pia mbinu za kuikabili nazo huwa haziko nyuma.

Hapo zamani teknolojia ya stealth ilikuja baada ya kipindi cha uvumbuzi wa rada ambapo wataalamu mbalimbali waliweza kuzisoma rada na kuchunguza tabia zake ili kuweza kukabiliana nazo na kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kufanya hivyo.

Lakini, kadri muda na miaka inavyozidi kwenda, teknolojia inabadilika na inalazimu kuachana na baadhi ya mbinu ama nyenzo. Mfano tu hata hiyo ndege ya F-117A ni teknolojia ya miaka ya 70 ambayo kwa kipindi cha baada ya miaka 20 au 25 haiwezi tena kuwa na ubora uleule wa awali kuendena na jinsi teknolojia ilivyokuwa miaka ile.

Inapelekea sasa kuwepo ulazima wa kuingia katika uwekezaji mkubwa wa kuweza kuboresha teknolojia katika viwango vyenye ubora zaidi kuendena na wakati na hapo sasa kuna uhitaji wa tafiti na rasilimali nyingi. Kuwa stealth dhidi ya adui kumekuwa ni moja ya vipaumbele vikubwa katika majeshi kwa miaka mingi sana na kutokana na hilo, mataifa makubwa kijeshi yamekuwa katika uwekezaji mkubwa wa teknolojia hii hivi sasa.
 
Nimekubali mkuu umetendea haki.. Ila tukirudi katika jaribio la kupunguza hiyo RCS unasemaje kuhusu matumizi ya material aina ya composite?
 
Stealth ni balaa Sana asante mkuu.
 
Nimekubali mkuu umetendea haki.. Ila tukirudi katika jaribio la kupunguza hiyo RCS unasemaje kuhusu matumizi ya material aina ya composite?
Nakushukuru kwa kuisoma makala hii.

Katika kupunguza Radar Cross Section kuna mbinu nyingi na hapa nimeelezea mbinu mojawapo kwanza. Katika muendelezo, tutapata kufahamu mbinu nyinginezo zitumikazo pia katika kupunguza Radar Cross Section.
 
Thank you nimeokoteza kidogo

Niliwahi Soma kidogo maswala ya anga Kama masomo ya ziada.
Tho I'm not interested kiasi hicho
Kisses[emoji8]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…