steers mjini pango la wanyang'anyi

steers mjini pango la wanyang'anyi

DOOKY

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
370
Reaction score
50
Wana JF nimebahtika kupita Steers hapa mjini.zamani ilikuwa sehemu safi ya kutoka na mtu wako wa karibu ile leo imezungukwa na wauza mitumba ya batiki na vinyago kila meza. Pana boa kwa kweli.
 
Wana JF nimebahtika kupita Steers hapa mjini.zamani ilikuwa sehemu safi ya kutoka na mtu wako wa karibu ile leo imezungukwa na wauza mitumba ya batiki na vinyago kila meza. Pana boa kwa kweli.
Kwahiyo wauza batiki na vinyago ndio "wanyang'anyi"?

Wajasiria mali tunanyanyapaliwa sana!
 
Wana JF nimebahtika kupita Steers hapa mjini.zamani ilikuwa sehemu safi ya kutoka na mtu wako wa karibu ile leo imezungukwa na wauza mitumba ya batiki na vinyago kila meza. Pana boa kwa kweli.

Ni kweli kabisa, sasa hivi kuna vendors kuzunguka eneo lile,taabu ni pale vendor anapofika mezani kwenu na kuwahamisha kwa muda ktk mtiririko wa mambo yenu/yako.

Uhuru uwepo,lakini mipaka iwepo pia. Itafika siku jamii itakosa hata sehemu nzuri ya kawaida ya kupumzika.
 
Kupaita pango la wanyang'anyi si sahii labda tu namna mambo yanavyokwenda pale yamebadilika tofauti na zamani ambapo mtu ulikuwa ukienda kukaa na kupata msosi unakutana na utulivu wa kutosha tofauti na sasa
 
du nimemshangaaa kupaita hivyo, ulikuwa umeiba kitu cha watu hukutaka kuonekana nini? au uliyekuwa na miahadi naye kakataa kuja baada ya kuona watu wengi?
 
Wana JF nimebahtika kupita Steers hapa mjini.zamani ilikuwa sehemu safi ya kutoka na mtu wako wa karibu ile leo imezungukwa na wauza mitumba ya batiki na vinyago kila meza. Pana boa kwa kweli.

Badilisha heading basi maana unapotosha kwa sisi ambao tunakula na kunywa hapo
 
Mkubwa badilisha Heading Tu Kaka, lakini ujumbe uliotaka kuwasilisha umefika. Sehem kama ile inatakiwa iwe utulivu mkubwa, mwingine anakwenda pale kutulia, sasa anapokutana na makelel kama bar inavunja moyo sana. Machinga wawe na kikomo, si mpaka mezani kusumbua mtu aliyetulia zake!
 
Sorry I was quoting the Bible verse when Jesus says my house will be a house of prayer not robbery
 
Ni kweli heading siyo nzuri kwa wajasiriamali; lakini hebu tuangalie huu mfumo wa ujasiriamali wetu unapoelekea maana sasa siyo ujasiriamali bali inaanza kuwa ni fujo. Kwa sasa kila mahali kumekuwa na biashara za mikononi, kweli hii ndiyo maana ya ujasiriamali. Ukipanda kwenye basi utakuta watu wanauza bidhaa, maofisini zinapitishwa bidhaa mikononi, ukiwa mahali unapata chakula mara umeletewa bidhaa; mimi huwa nashindwa kuelewa hivi watu wakati wote huwa wanatembea na pesa kununua chochote tu kitakachokuwa mbele yake. Hivi tatizo ni nini? Je tunakosa muda wa kwenda kutafuta mahitaji yetu. Kwa uzoefu nimegundua kwamba hivi vitu vinavyouzwa mikononi wakati mwingine huwa bei iko mara mbili ya bei halisi. Nafikiri iko haja ya kupitia mifumo yetu ya biashara la hasha huko mbele itakuwa balaa.
 
Back
Top Bottom