NGOMEKONGWE2021
JF-Expert Member
- Dec 6, 2021
- 616
- 1,225
Wadau,
Kama mtumiaji wa mara kwa mara wa stendi hizi kuna mambo ambayo najiuliza kwamba hawa jamaa waliojenga stendi ya Magufuli imekuwaje wamejenga stendi ambayo sifa yake ni lile ghorofa tu lakini kwa ujumla wake haikidhi mahitaji ya abiria . Rais asingekubali kuizindua na jina lake kutumika ila walimchomekea kwa kumuonyesha lile ghorofa hivyo akaingia mkenge na kulizindua. Yafuatayo ni mapungufu ninayo yaonaga nikilinganisha na stendi ya Dodoma;
A. STENDI YA MAGUFULI
B. STENDI YA DODOMA
Sasa huwa najiuliza walliojenga ya DAR walikwama wapi?
Standi ya mabasi Dodoma
Standi ya mabasi ya Magufuli

- Uingiaji wa mabasi ni wa hovyo
- Sehemu za abiria kusubiria mabasi hazipo zinapotakiwa kuwepo, kama basi limechelewa na upo eneo la kuondokea, manake inabidi usimame wima manake huwezi kwenda kule ghorofani ambako ni mbali na pia huenda usilione basi lako linavyoingia
- Vyoo ni vidogo, muda wote vimeloa maji na vichafu, vina foleni, halafu vimekaa mbali na abiria
- Sakafu inaposimama mabasi ni ya hovyo
- Kwa ujumla mazingira ya pale ni ya hovyo labda lile ghorofa ndiyo linaonyesha kuna kitu kimefanyika
- Uingiaji wa abiria hasa ukiwa na private car haueleweki na ni wa hovyo
B. STENDI YA DODOMA
- Kuna mpangilio mzuri wa uingiaji na utokaji mabasi
- Kuna mpangilio mzuri wa uingiaji wa watu
- Kuna space kubwa kiujumla kwa kila kilichopo
- Vyoo vina nafasi kubwa na visafi sana
- Structure imejengeka vizuri na hawakulipua
- Kuna mpangilio mzuri wa maeneo ya kusubiria mabasi
Sasa huwa najiuliza walliojenga ya DAR walikwama wapi?
Standi ya mabasi Dodoma
Standi ya mabasi ya Magufuli