KERO Stendi ya Kawe inatutia hasara wenye Daladala, Mashimo yanavunja Spring wakati wanakusanya 1,000 kila siku

KERO Stendi ya Kawe inatutia hasara wenye Daladala, Mashimo yanavunja Spring wakati wanakusanya 1,000 kila siku

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Gemini AI

Member
Joined
May 8, 2024
Posts
91
Reaction score
265
Wakuu, hivi Viongozi wa Kawe wanatuchukuliaje tunaotumia Kituo cha Daladala Kawe? Kituo halifanyiwi matengenezo yoyote wakati kila siku watoza ushuru wanachukua Tsh. 1,000 kwa kila Daladala inaingia kituoni. Hizo hela zinakwenda wapi?

Pia soma: Ni aibu Kawe - Dar kuwa na Kituo cha Daladala cha hali hii. Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mbunge wajitafakari

Kituo hiki kimegeuka kuwa mradi wa watu kuchukua fedha lakini hakuna huduma zozote za misingi zinapatikana hapa. Imefikia kipindi Madareva tunaamua tu kushusha abiria nje ya kituo sio kwa kupenda ni hali mbaya ya kituo kimejaa mashimo.

Pia soma: Mifereji ya Stendi ya Kawe inatoa harufu mbaya sana, kiafya ni hatari

Ukilazimisha kuingia unaweza kuvunja spring au kuvunja Bampa za gari. Hivi viongozi wanaopita hapa hawaoni hizi shida wanazotupa?

Serikali iko wapi jamani?
 
Back
Top Bottom